MWANADADA Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa
katika maisha yake hawezi kuwasahau watoto yatima na kuanzia sasa, kila
mwaka lazima asherehekee nao katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.
Odama ambaye hivi karibuni alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa
na kutoa misaada ya vyakula na vitenge kwa watoto yatima na walezi wao
wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar huku akiangusha sherehe ya
nguvu ndani ya ukumbi wa Vijana na kuungana na watoto hao, alisema huu
ni wakati wa watoto kufurahi naye.
“Nimeshasherekea sana bethdei baa na marafiki zangu, lakini kwa sasa
nimebadilika na ndiyo nimeanza mwaka huu nitakuwa na watoto yatima kila
mwaka nikikumbuka siku yangu ya kuzaliwa kwani kama hivi wamejisikia
faraja sana kuja kula pamoja na mimi, kucheza muziki pia kuwaona
waigizaji mbalimbali imekuwa ni furaha kwao,”
Wednesday, September 10, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» MTOTO MZURI ODAMA WA BONGO MOVIE NA MAWAZO YA BUSARA ZAIDI..
0 comments:
Post a Comment