Taarifa
zimethibitishwa kuhusu staa wa hit single kama ‘pombe yangu’ ‘tema mate
tuwachape’ na ‘ni shidaah’ Madee ambae ni msanii kutoka kundi la TipTop
Connection kushikiliwa na Polisi.
Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo ambae ni Babtale
, Gossip Cop
Soudy Brown kwenye You heard inayosikika kupitia XXL ya CloudsFM
J3-Ijumaa alisema ‘inasemekana Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu
yake na watu wawili usiku huko Kigamboni’
Babtale alipoulizwa akasema ‘Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee
wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye
pikipiki wakampora kwa hiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa
na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki alafu wakaigonga pikipiki kwa
nyuma, pikipiki ilivyodondoka yule aliekua nyuma kwenye pikipiki ambae
ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata
aliekua anaendesha hiyo pikipiki’
‘Wakamchukua
na kwenda nae maskani Tiptop… mama yake akaja akasema msipeleke Polisi
mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu, Madee kwa sababu
alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake…… saa nne asubuhi
yule mama akaja na Polisi badala ya kuja na mwizi mwenzake akaja na
Polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop,
walimchukua huyo Muhalifu kwenye Land rover mpaka Polisi Magomeni na
kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa’
‘Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka Hospitali,
nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa Polisi akaripoti…. kufika
kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka
Hospitali akawaambia huyu ni mwizi ameiba, ikabidi Dogo aingizwe ndani
jana akalala pale Polisi Magomeni’
‘Asubuhi
yake Madee akaenda kituoni kama kufata Mwalifu wake na kutaka simu yake
aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe Kigamboni…. saa kumi na
mbili jioni ndio Kwebe ananitumia msg anasema Madee analalamika mbona
humfatilii nikauliza kuna nini tena akasema wamemuingiza ndani, nikapiga
simu Polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako tulitaka kumtoa
lakini hatuwezi sababu amemteka mtu, nikapiga simu kwenye vyanzo vyangu
vya msaada tukamtolea dhamana…. ni hilo
USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI PIGA NO. 0712473752
Wednesday, September 24, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Sababu za Madee kushikiliwa na Polisi.. chanzo ni hiki cha jamaa wawili wa Pikipiki
0 comments:
Post a Comment