Search This Blog

Monday, September 22, 2014

Video: Lampard Asema Kilichomzuia Kushangilia Bao La Kuiokoa Man City

Video: Lampard Asema Kilichomzuia Kushangilia Bao La Kuiokoa Man CityKiungo kutoka nchini Uingereza Frank Lampard ametoa sababu ya kwa nini alishindwa kushangilia mara baada ya kuiwezesha klabu ya Man City kupata bao la kusawazisha wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Chelsea hapo jana.
Lampard, amesema ilikuwa ni vugumu kwake kushangilia bao alilofunga kutokana na mapenzi ya dhati aliyo nayo dhidi ya klabu ya Chelsea ambayo ilimtunza kwa miaka 13 iliyopita akitokea West Ham utd.
Lampard, amesema bado anaipenda klabu hiyo na siku zote anahisi ni sehemu ya maisha yake hivyo hawezi kuiumiza nafsi yake kutokana na mazingira aliopo sasa ambayo ni tofauti na klabu hiyo ya magharibi mwa London.
Amesema ni vizuri kwake kufanya kazi kwa uadilifu na anatambua uweledi uliopo kutokana na uwajibikaji wake anapokuwa uwanjani hususan inapotokea anacheza dhidi ya klabu anayoipenda.
“Naamini sijakosea na wala sijamkwaza yoyote, nimetimiza wajibu wangu ndani ya uwanja na suala la kushangilia ama kutoshangilia lilikuwa ndani ya maamuzi yangu hivyo ni jambo la kawaida.” Amesema Lampard
Lampard, anaitumikiwa klabu ya Man city kwa mkopo akitokea nchini Marekani ambapo alisajiliwa na klabu ya New York City FC miezi miwiwli iliyopita baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Chelsea.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 aliondoka Chelsea huku akiwa ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora kwa wakati wote wa klabu hiyo baada ya kufunga mabao 211 katika michezo 648 aliyocheza akiwa Stamford Bridge.

0 comments:

Post a Comment