RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili
wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Jijini Dar Es Salaam na kutiwa saini na Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza
Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa
Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa
mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Saturday, September 20, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Kikwete amteua Mh.Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
0 comments:
Post a Comment