Search This Blog

Wednesday, September 24, 2014

Ronaldo Bado Kidume La Liga, Apiga Nne Mguuni Mwake

Ronaldo Bado Kidume La Liga, Apiga Nne Mguuni MwakeMshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro ameendeleza ushajuaa wa kuisaidia klabu ya Real Madrid kupata ushindi katika mchezo wa pili mfululizo wa ligi ya nchini Hispania msimu huu.

Ronaldo alidhihirisha ushujaa wake wakati wa mchezo wa ligi hiyo uliochezwa Estadio Stantiago Burnabeu usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Elche.
Katika mchezo huo mshambuliaji huyo ambaye anashikilia tuzo ya uchezaji bora wa dunia alifanikiwa kufunga mabao manne pekee yake huku bao moja ambalo lilihitimisha ushindi wa mabao matano likifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Wales Gareth Bale.

Hata hivyo Edu Albacar aliiongoza Elche, kupata bao la mapema katika dakika ya 15 kwa njia ya mkwaju wa penati, lakini pamoja na juhudi hizo bado mambo yaliwageukia na kujikuta wakibanjuliwa kwa kipigo cha aibu.
Mchezo mwingine wa ligi ya nchini Hispania uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo ulishuhudia Deportivo de La Coruña wakiendeleza uteja katika ligi hiyo kwa kufungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Celta de Vigo.
Hii leo ligi ya nchini Hispania inaendelea tena kwa michezo kadhaa kuchezwa ambapo;
Almería v Atl Madrid
Eibar v Villarreal
Rayo Vallecano v Ath Bilbao
Granada CF v Levante
Málaga v Barcelona
Sevilla v Real Sociedad

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

0 comments:

Post a Comment