Siku
hizi mapenzi yamekua kama karata hivyo kila mmoja anacheza ajuavyo au
awezavyo kwenye huu uwanja mpana ambao kwa kiasi kikubwa miaka
inavyosogea ndio vifo vingi hutokea kutokana tu na visa vya mapenzi.
Taarifa kutoka Dodoma na kuthibitishwa na Polisi, zinahusu Wananchi
kupatwa na hasira na kumuua Mwanaume aliyemuua mke wake kwa kumpiga na
rungu tumboni kwenye kijiji cha Mzogole.
Mwanamke aliyeuwawa ana umri wa miaka 48 Mwajuma Chomola na mume wake
ambae ndio mtuhumiwa ana umri wa miaka 55 anaitwa Richard Kodi ambapo
kwa mujibu wa gazeti la HabariLEO, Mwanaume huyu alifariki dunia wakati akihudumiwa hospitali ya wilaya ya Mpwapwa.
Wakati uchunguzi ukiendelea, matokeo ya awali yanaonyesha chanzo cha
yeye kumuua mke wake waliekua wakiishi pamoja ni wivu wa kimapenzi na
kwamba ishu ilianzia pale Mwanamke alipochelewa kurudi nyumbani akitokea
kwenye sherehe iliyofanyika kwenye kijiji hichohicho wanachoishi lakini
mume alidhani mke kaenda kwengine.
Yaani sio kwamba alimfumania bali alihisi tu mke wake kaenda kwengine
ndio sababu iliyomfanya akachukua haya maamuzi, mara nyingi kwenye
mapenzi kumekua na kesi nyingi zinazosababisha Wanawake kupigwa au
kuuwawa kwa sababu tu Mwanaume anahisi vitu kama hivi bila kuwa na
ushahidi.
Tuesday, September 23, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Visa vya mapenzi haviishi…. huyu wa Dodoma kamuua mke kwa rungu, chanzo?
0 comments:
Post a Comment