Mdau wa
Sanaa Henry Mdimu (Kulia) akisisitiza umuhimu wa kuwa na mitandao ya
kijamii kwa wasanii (hawapo pichani) katika Jukwaa la Sanaa la Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA). Kushoto ni Afisa Sanaa wa BASATA, Augustino
Makame.
Afisa
Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kulia)
akisisitiza jambo kwa Wasanii (Hawako pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa
lililofanyika mapema wiki kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala,
Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau wa Sanaa Henry
Mdimu na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.(P.T)
Wadau wa
Sanaa pamoja na Wasanii wakipata elimu kuhusu Nafasi ya Mitandao ya
Kijamii katika Kukuza Sekta ya Sanaa kwenye mapema wiki hii kwenye
Jukwaa la Sanaa la BASATA.
Na Mwandishi Maalum
Wasanii wamesisitizwa juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani waandaaji wa matamasha na matukio mbalimbali ya kisanaa sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiitumia katika kuwapa kazi.
Wasanii wamesisitizwa juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani waandaaji wa matamasha na matukio mbalimbali ya kisanaa sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiitumia katika kuwapa kazi.
Akizungumza
kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar
es Salaam, mdau wa Sanaa Henry Mdimu alisema kuwa ni jambo la kushangaza
kuona wasanii wakitumia kurasa zao kuonesha mambo binafsi kama ya
mapenzi na matusi wakati zinapaswa kutumika kwa ajili ya kazi zao za
Sanaa na kuwasiliana na mashabiki wao.
Alisisitiza
kwamba si kila kitu kinapaswa kuwekwa kwenye kurasa za kijamii za
wasanii na kwamba lazima wasanii wajifunze kutenganisha maslahi au
masuala yao binafsi dhidi ya yale ya wapenzi wao na kwamba Sanaa iko kwa
ajili ya walaji na si wasanii pekee.
“Wasanii
hawana budi kuelewa kuwa hawatengenezi sanaa au kurasa za mitandao ya
kijamii kwa ajili yao. Wanaitengeneza ili kuwasiliana na mashabiki wao
kuhusu kazi wazifanyazo na kutafuta fursa za masoko na kazi nje. Lazima
waelewe mapromota wa kimataifa hutumia sana kurasa hizi katika kutoa
fursa” alisisitiza Mdimu.
Aliongeza
kwamba, msanii yeyote anayefanya kazi ya Sanaa kama kazi yake lazima
afikirie kutumia mitandao hii ya kijamii kiweledi katika kujitangaza
kwani kutokufanya hivyo ni bora kufanya kazi nyingine maana hiyo ndiyo
njia kuu kwa sasa ya kujitangaza na kupata fursa za maonesho mbalimbali
ya kimataifa kwa gharama nafuu.
Kwa
upande wake Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame alisema kwamba
Baraza limekuwa mstari wa mbele kusisitiza matumizi sahihi ya teknolojia
za kupashana habari muiongoni mwa wasanii na kwamba sasa ni muda wa
wasanii kuona umuhimu wa mitandao hii ya kijamii na kuitumia ipasavyo
katika kukuza Sanaa zao.
USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA
0 comments:
Post a Comment