Kama wewe ni mmoja kati ya ‘waliodata’ na ngoma ya Linah aliyofanya
Afrika Kusini akiwashirikisha Uhuru, tegemea kudata zaidi na ujio mpya
wa msanii huyo.
Linah ambaye hivi sasa anafanya kazi chini ya kampuni ya kimataifa ya
‘No Fake Zone’, ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa wimbo unaofuata
utakuwa mkubwa zaidi ya Ole Themba na kwamba amefanya na msanii mkubwa
sana Afrika.
“Yaani inakuja kubwa zaidi ambayo hiyo itakuwa funika, waswahili
wanasema itakuwa ‘ndio basi tena..’ (anacheka). Nimeshaifanya ila kuna
baadhi ya vitu ambavyo naenda kumalizia. Kwa hiyo Mungu akijalia hizo
wiki zinazokuja ntaenda (Afrika Kusini) kumalizia.” Linah ameiambia
tovuti ya Times Fm.
Hata hivyo hakumtaja msanii huyo aliyefanya nae kazi na kuahidi kuwa
itakuwa surprise baada ya kazi kumalizika na kutoka kama ilivyokuwa ‘Ole
Themba’.
Katika hatua nyingine, Linah ameeleza kuwa wimbo wake Ole Themba
umempa mafanikio makubwa ambayo hakuwahi kuyafikia na kwamba sio
Tanzania tu bali Afrika kwa ujumla kwa kuwa video yake imechezwa katika
vituo vingi sana vikubwa.
Usikose kusikiliza Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm Jumamosi hii
kuanzia saa 10 kamili jioni utamsikia Linah akieleza mengi ikiwa ni
pamoja na ufafanuzi baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa wanawake na
Uchumi.
Friday, September 19, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Ulidata na Ole Themba? Linah anakuja na wimbo mkubwa zaidi, amshirikisha msanii mkubwa Afrika
0 comments:
Post a Comment