Mhe.
Waziri Fatma Fereji akiwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan
Mwinyi wakati wa ufunguzi wa Kikao Maalum wa ICPD ambapo Waziri Fereji
aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo.
Kutoka
kushoto ni Balozi Ramadhan Mwinyi, Waziri Fatma Fereji wakiwa na
Mwakilishi kutoka Ofisi za UNFPA ambaye aliwahi pia kufanya kazi nchini
Tanzania akimpongeza Waziri baada ya kutoa mchango wa Tanzania na kulia
kabisa ni Dkt. Joyceline Kaganda.GPL(P.T)
Mhe.
Waziri Fatma Fereji kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar akizungumza kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa Kikao Maalum cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa
kilichofanyika Jumatatu ambapo wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali
kutoka nchi 193 walikutana kutathimini Mpango wa Utekelezaji
walioupitisha miaka 20 iliyopita huko Cairo, Misri kuhusu uboreshaji wa
maisha ya watu na masuala yahusuyo Idadi ya Watu. Mhe. Fereji ni sehemu
ya Ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa 69 wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA
0 comments:
Post a Comment