Kocha wa Chelsea Jose Morinho amesema timu yake
haikutumia vema pengo la mchezaji mmoja wa Manchester city aliyetolewa
kwa kadi nyekundu kwakuwa mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao moja
kwa moja ulikuwa mgumu na wenye hisia kali.
Katika mchezo huo
uliochezwa kwenye dimba la Etihad siku ya jumapili, mchezaji wa zamani
wa Chelsea Frank Lampard ndiye aliyeiokoa Man City kutoka kwenye hatari
ya kuziacha pointi zote tatu kwa Chelsea huku vijana hao wa Manuel
Pelegrin wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya Pablo Zabaleta
kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 66.Wakati hayo yakijiri Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini, amebeza mbinu za mpinzani wake Mourinho katika mchezo huo kwa kusema kuwa Vijana wake wa darajani walicheza kama timu ndogo na kukosoa mtindo wao maarufu wa kupaki basi…
0 comments:
Post a Comment