Wakati
Mbunge Steven Ngare akikagua mradi wa maendeleo kwenye shule ya msingi
huko Kenya kuna jamaa alijitokeza na kujaribu kutaka kumvamia ili
amkatekate kwa panga lakini kabla hajamfikia tayari mlinzi wa mbunge
akawa amemuona.
Imetokea kwenye kijiji cha Kariti kaunti ya Kainyaga huko Kenya
ambapo baada ya mlinzi kuona na kupata uhakika jamaa huyo alikua na nia
mbaya, alichukua bastola yake na kumpiga risasi tatu zilizosababisha
mwanaume huyo kufariki papohapo huku sababu zaidi za kwanini alitaka
kufanya hivyo zikiwa hazijulikani.
Kwa mujibu wa Citizen TV, mtu huyu alitaka kumshambulia mbunge huyu
muda mfupi tu baada ya kumkata kwa panga mwalimu mkuu wa shule hiyo
kulikompa majeraha na kumfanya awe mahututi hospitalini hadi sasa.
NYINGINE
Taarifa nyingine kutoka Radio Jambo ya Kenya ni kuhusu hii ya
mshukiwa mkuu wa mauaji ya Mbunge aitwae George ambae alifariki baada ya
kunywa kinywaji kilichowekewa sumu, amepoteza kwa mara nyingine tena
ombi la kutaka kuachiwa kwa dhamana kwa sababu alizozitoa kwamba ana
matatizo ya kiafya.
Paul Wainaina ni mmiliki wa Baa ambako inadaiwa marehemu Mbunge George ndiko alikowekea sumu kwenye kinywaji chake.
NYINGINE:
Malipo ya umeme yatapungua nchini Kenya mwezi huu kutokana na
kuanzishwa kwa miradi mingi zaidi ya kuzalisha umeme ambapo kampuni
husika imesema huenda malipo hayo yakapungua kutoka shilingi 17 za Kenya
mpaka shilingi sita kwa kilowati moja ambapo pia serikali ya nchi hiyo
inajitahidi kufanikisha mradi wake wa kuongeza megawati elfu 5 za umeme
kufikia mwaka 2017.
USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI PIGA NO. 0712473752
Wednesday, September 24, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Risasi alizopigwa jamaa alietaka kumuua Mbunge kwa panga.
0 comments:
Post a Comment