Katika mchezo wa tenesi mchezaji Victoria
Azarenka raia wa Belarus atakosa sehemu iliyobaki ya msimu wa mchezo huo
kutokana na jeraha la mguu ambalo limeharibu mwaka wake Mchezaji huyo
ambaaye ni mshindi mara mbili katika mashindano ya Australian Open
amekwisha kosa miezi mitano katika mwaka huu pekee na kuporomoka kutoka
nafasi ya pili mpaka ya 25 katika viwango vya dunia vya mchezo huo.
Azarenka
mwenye umri wa miaka 25, alifika robo fainali ya US open mwanzoni mwa
mwezi huu na alipangwa kurejea uwanjani katika mashindano ya Wuhan Open
huko China.
0 comments:
Post a Comment