Ukraine ,Poland na Lithuania zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja litakaloshirikisha maelfu ya wanajeshi.
Akizungumza
baada ya mataifa hayo matatu kutia sahihi makubaliano hayo mjini
Warsaw,rais wa Poland Bronislaw Komorowski amesema kuwa jeshi hilo
linatarajiwa kufanya zoezi lake la kwanza la kijeshi mwaka huu na kwamba
litashirikisha oparesheni za kulinda amani.Kitengo hicho cha jeshi kitakuwa na makao yake makuu katika mji wa mashariki mwa Poland Lublin,ikiwa ni kilomita chache kutoka mpaka wa Ukraine.
Mpango wa Jeshi la pamoja ulianzishwa mnamo mwaka 2007 ,na sasa unaonekana kupigwa jeki na wasiwasi uliozushwa na jeshi la Urusi katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment