Search This Blog

Tuesday, September 23, 2014

Video: Hatimae Beyonce aonyesha picha yake akiwa na mimba ya Blue Ivy amepozi mtupu na Jay z, Video ya harusi yao ambayo haikuwahi kuonekana popote...

Baada ya tetesi kibao kusambaa juu ya ndoa yao wengi wakidai kuwa ipo mashakani na hata kusemekana kuwa si kweli kuwa Beyonce ndie aliemzaa Blue Ivy, Beyonce na Jay Z wamejaribu kuzizima tetesi hizo baada ya kujumusiha video zao binafsi (home videos) wakati wa usiku wa mwisho wa tua yao pamoja "On The Run Tour"
Kipande hicho cha video chenye dakika 6 kilionekana kwenye background wakati wawili hao wakiimba hit song zao "Young Forever" na "Halo" wakionekana katika sehemu mbali mbali waki-enjoy wakati wa mapunziko, wakiwa kwenye boat na ku -share champagne.
Video ya siku ya harusi yao(2008) ambayo haijawahi kuonekana imechanganywa katika mix ya video hizo pia video ya wawili hao wakichora tattoo zinanofanana kwenye vidole vyao


 Video hiyo iliendelea kuonyesha video ya karibu ya ujauzito wa Beyonce akiwa mtupu mbele ya Jay Z huku Jay akiwa amekunja mikono yake mbele ya tumbo la Bey.hata kuna vipande vya hospitali vinavyomuonyesha Bey akiwa amempakata mtoto wake dakika kadhaa baada ya kujifungua.
Akiongezea juu ya tetesi zinazoendelea, Jay alibadilisha mashairi ya wimbo wake Beach Is Better, kutoka "I replace it with another one" na kuwa "Cause she is pregnant with another one" wakati huo huo sio Bey wala Jay wamethibitisha kuwepo kwa ujauzito wa mtoto wa pili.
Wawili hao walimaliza tour yao na show mbili za Paris zilizokuwa sold out.
 
 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

0 comments:

Post a Comment