Search This Blog

Monday, September 22, 2014

Florenzi Ashangilia Kwa kumbusu Bibi Yake Jukwaani

Video: Florenzi Ashangilia Kwa kumbusu Bibi Yake JukwaaniKiungo wa klabu ya AS Roma ya nchini Italia Alessandro Florenzi, usiku wa kuamkia hii leo alidhihirisha namna anavyompenda bibi yake kipenzi wakati akushangilia moja ya mabao ya klabu hiyo iliyokuw ana kazi ya kupambana na Cagliari.
Florenzi alionyesha hatua hiyo kwa kumkimbia bibi yake aliyekuwa jukwaani akimfuatilia uwanjani na kumbusu huku akichelea kwa furaha kutokana na bao muhimu aliyoifungia klabu yake ambayo ilichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Wakati anaelekea jukwaani mashabiki waliokuwa wamehuhuria uwanjani hiyo jana walikuwa hawatarajii kama kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 angeweza kufanya kitendo hicho, lakini iliwezekana kwa mshangao mkubwa.
Mshabiki walishikwa na hali ya taharuki na hatimae kuishia na vicheko vya furaha baada ya kumuona mchezaji huyo akikimbia jukwaani na kupanda ngazi na hatimae alimkumbati bibi yake kipenzi na kumbusu kwa furaha.
Hata hivyo kitendo hicho kilimsababishia Florenzi kuonyeshwa kadi ya njano kutokana na kuvunja sheria za mchezo wa soka ambazo huwazuia wachezaji kushangilia kwa kujumuika na mashabiki, kwa kuhofia hali za usalama wao.
Bao la kwanza la AS Roma katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Italia Mattia Destro katika dakika ya 10 na dakika tatu baadae Alessandro Florenzi alifunga bao la pili.

0 comments:

Post a Comment