Search This Blog

Monday, September 22, 2014

Abbott ''Usalama wetu unatangulia uhuru ''

Waziri mkuu wa Australia ,Tonny Abbott amesema sheria mpya za kupambana dhidi ya ugaidi zilizopendekezwa zinasema kuwa itakuwa hatia kwa raia wa Australia kujiunga na makundi yenye itikadi kali.
Amesema kuwa raia yeyote atakayeshiriki katika ugaidi atakabiliwa na mashtaka na hukumu ya mda mrefu jela iwapo atarudi nyumbani Australia.
Iwapo pendekezo hilo litaidhinishwa itakuwa rahisi kwa maafisa wa polisi kuwachunguza na hata kuwazuia washukiwa wa ugaidi mbali na kuharamisha raia wa Australia kusafiri kwenda maeneo yanayomilikiwa na wanamgambo.
Hatua hiyo inafuatia oparesheni kali ya kiusalama wiki iliyopita ambayo serikali inasema ilitibua njama za kundi la wanajihad kutekeleza mauaji ya kiholela nchini Australia.
Inaaminika kuwa takriban raiya 60 wa Australia wanapigana miongoni mwa wanamgambo wa kiislmu wa Islamic State nchini Syria na Iraq.
Abbott :Wakati umewadia kwetu kulinda maslahi ya taifa kabla ya Uhuru
Bwana Abbott alitaja mji wa Raqqa ulioko kaskazini mwa Syria kuwa mfano wa miji ambayo itapigwa marufuku kwa Waaustralia kwenda huko .
Kauli hiyo inafuatia picha ya kijana mmoja raiya ya Australia iliyochapishwa kwenye mtandao wa Intanet akiwa ameshika kichwa cha askari wa Syria kilichokatwa.
Kijana huyo inaaminika ni mwanawe mwanamgambo wa Islamic State ambaye ana uraiya wa Australia.
''Sheria hiyo mpya itasaidia sana kuwaondoa magaidi mabarabarani mwetu na kuwafungia kwa kipindi kirefu mno''
Ningependa iwe wazi kuwa hatutakubali kamwe magaidi waishimiongoni mwetu''
''Nafkiri wakati umewadia wa kuweka usalama mbele ya Uhuru kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa letu''
alisema bwana Abbott.

0 comments:

Post a Comment