Search This Blog

Saturday, September 20, 2014

Kwanini lawama kwapromota haziwezikumwepushaDiamond kupotezamashabiki

  1. Kutofanyika kwa show ya kimataifa
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na
mashabiki wengi wa Diamond jijini
Stuttgurt, Ujerumani na kusababisha
uharibifu mkubwa, kulichukuliwa na
watu wengi kama ajali kazini.
Sababu za Diamond kuchelewa
kupanda stejini kulikotokana na kudai
alipwe fedha yake iliyokuwa imesalia
kwa promota, ilikuwa ya msingi
kabisa. Na pia kampuni yenyewe
iliyoandaa show hiyo ilieleza kwa
urefu kilichosababisha na pia kuahidi
show ya bure kwa mashabiki wa
Diamond.
Hilo lilipita na kila upande ukaganga
yajayo. Ijumaa hii Diamond alikuwa
afanye show nyingine jijini London,
Uingereza. Bahati mbaya show hiyo
ambayo yeye mwenyewe kama
kawaida yake aliipigia promo sana,
haikufanyika. Kama ilivyokuwa ya
Ujerumani, mashabiki walimsubiri staa
huyo kwa masaa kibao wasimuone
akitokea. Baada ya kuonekana
kunakucha bila dalili ya Diamond
kupanda jukwaani, wengi walianza
kudai warudishiwe fedha zao. Na kwa
mujibu wa mtu aliyekuwepo kwenye
show hiyo, polisi walisaidia kurejesha
amani katika ukumbi huo, lasivyo
yangetokea kama ya Ujerumani.
Pia anadai kuwa promota wa show
hiyo alikamatwa.
“I was there brov it was maad trust
me, even police got involved with that
shit, they had to calm people down
until seven in the morning, people
wanted their money back he I’ll pay
the price cause he got arrested,”
ameandika.
Diamond amemtupia lawama
promota huyo ambaye si mara ya
kwanza kufanya naye kazi na kumuita
tapeli.
“Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!
….kuweni makini sana na promoter
huyu (Victor – Dj rule) mnaposikia
kaandaa show, party au Hafla
yoyote…ni vyema kuziepuka na
kutohudhuria kabisa kwasababu ni
tapeli…. si unajua aisifiae mvua
imemnyeshea… basi mie nimeloa
kabisa.”
Pamoja na kwamba Diamond hana
makosa katika hili, hawezi kukweka
lawama kutoka kwa mashabiki wake
walio na kinyongo naye. Shabiki
hatotaka kujua makubaliano kati ya
msanii na promota. Anachojua yeye ni
kuwa show ilitangazwa kuwa
itafanyika na yeye akanunua tiketi kuja
kushuhudia.
Si kazi yake kutaka kujua kama msanii
amelipwa fedha yake ama lah! Kama
Diamond alikuwa anamfahamu vyema
DJ Rule kuwa si mwaminifu, kwanini
alikubali kufanya naye show? Sijui
makubaliano yao yalikuwa vipi, lakini
kwanini alikubali kulipwa fedha nusu
kabla ya kutumbuiza?
Ni yaleyale kama ya Ujerumani.
Wengi tunamchukulia Diamond kama
mfano wa msanii wa Tanzania
aliyefanikiwa na tunategemea kuwa
makubaliano yake yanapaswa kuwa
kwamba promota anatakiwa kumlipa
ama fedha nusu, robo tatu au fedha
yake yote (kama anamuamini) na
kusaini mkataba unaowafunga wote.
Mara nyingi mikataba husema fedha
iliyosalia inatakiwa imfikie msanii wiki
moja ama siku chache kabla ya show.
Wengine hukubaliana fedha hiyo
alipwe msanii pindi anapowasili katika
mji huo ama anapofika hoteli.
Ninafamu kuwa Diamond na timu
yake wako smart mara nyingi lakini
nashindwa kupata jibu la kwanini
makosa kama haya yanaendelea
kutokea tena katika show za kimataifa.
Kuna uwezekano mkubwa kama
hajapoteza mashabiki wengi, basi
heshima waliyokuwa nayo kwake
imepungua.
Yeye na timu yake wanapaswa kuwa
smart na kusaini mikataba ya show
isiyokuwa na ahadi za kupeana fedha
iliyobaki siku ya show. Promota
wanapaswa kujipanga na
wanapotafutwa na promota wenye
longolongo wasiwe na aibu
kuwakatalia moja kwa moja kutunza
heshima yao.
Matukio kama haya yanaweza kuwa
mabaya kwa biashara pia kwakuwa
baadhi ya promota wa kimataifa
hawapendi kufanya kazi na wasanii
wenye CV mbaya katika show zao
zilizopita.
Haya ni baadhi ya maoni ya watu
mbalimbali yanayofanana kiasi na ya
kwangu.
kiswigogodfrey
Play back concert 2 times inabuma
hiyo ni kukosa management imara
yenye kusimamia mikataba yako.
Umetoka bongo hadi UK bila kujua
mikataba yako. Hilo fans wako
haliwahusu wao ni burudani ndio haki
yao hayo mengine utajijua na
promota wako. Na kama jamaa
amekupiga kama ulivyo post ni vzr
ukafuata taratibu za kisheria ndio zitoe
hukumu na ukishinda ndio umwanike
kwenye social network.Kama
hujafanya hivyo tegemea kesi ya
madai kutoka kwa mshikaji ingawa
umeshapata hasara kwa kukosa
umakini na management yako, it’s
over.
jamal_huwel
Men mara ya pili hii hebu badilisha
system ya mikataba yako. Pokea
angalau 60% of the cash kabla ya
shoo. Watakuharibia mtaalamu wetu
tutakosa talent yako tena
Allykikasha
PLZ PLZ PLZ READ THIS….DIAMOND
wewe ushakuwa msaani wa kimataifa
na watu nao wanakufahamu,, jaribu
kutafuta timu ya uhakika mtu anayejua
ishu ya marketing professionally,, uwe
na mwanasheri hata yule wa kumlipa
tu pale unapoingia mkataba,, achana
na waki BABU TALE wao umeneja wao
ni wa show za mikoani tuu,, then
hana creativity yoyote zaidi ya
kuwanufaisha,, jaribu now to change,,
uwe na watu wenye uwelewa na kitu
unachokifanya,, Germany imetokea ,,
then BAB TALE anasema eti imesaidia
kukutangaza,, very stupid comment
then ISSUE SIO PROMOTERS ITAFIKIA
SIKU FANS NOW WATAONA KILA
SHOWS ZAKO NI ZA KITAPELI ,, PEOPLE
THEY CHANGE.
carryandy
Acha kuwatangazia mashabiki wako
show kabla hujalipwa hela kamili,
vinginevyo unajiharibia biashara 2nd
time hii, hujajifunza tuu? Na sijui
kama unakuwa na makubaliano ya
maandishi kabla hujajiingiza
kuwambia fans wako utkuwa
somewhere. , jipange utaja pata
matatizo makubwa nchi za watu hizo
oh!
rayna_rayna_
Mmmhh um not sure kama anaweza
kukufanyia ivyo maybe umeenda bila
contract ndo mana imetkea yote..next
tym jipange na team yko najua jamaa
ni mtu mkubwa and also unaweza
kwenda mshitaki ubalozini kwa
kukupotezea mda na kukupotezea
issue maybe it will help
callyrissanen
Pia kuwa makini chibu. Hao police wa
nchi za wenzetu wakifanya
mawasiliano unaweza hata huko
germany ushindwe kufanya show.
Tafuta mwanasheria wa hiyo mikataba
yako. Na uwe unamaliziwa kulipwa
pesa za show unapofika tuu kwenye
nchi husika, msisubiri hadi muda wa
onyesho ndio muanze kudaiana.
Inakuwa rahisi kutoa tamko kwa
mashabiki mapema kama
hutohudhuria mapema iwezekanavyo
ili wasisumbuke
irymamur_de_star
Inaonekana management yako haipo
makini kabisa kwan inatokea nn??
hadi mtu anakutapeli cc mashabiki
zako tunaumia xana kuckia ivyo na
maswal mengi juu ya hilo kwan
thamani yako ya show za nje
inapungua xaxa kuwa makini na hao
bakoharam sio watu wazuri kwako na
huyu jamaa xaxa mi sioni kazi yake
@babutale mi nakupa pole xana
kwailo!!!! ila hujafafanua vzur juu ya
hilo tujue ilikuaje yani tujue mwanzo
mwisho kwa maelezo kwan tunahaki
kama mashabiki zako pendwa!!!!

0 comments:

Post a Comment