Ndugu wa
mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35) ambaye
ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa la
House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko
Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo kwa miezi
nane mfululizo. GPL(P.T)
Mwalimu Galus Focus Nguruwe akiwa amefungwa mnyororo
Kwa
mujibu wa dada wa Galus, Piencia Focus, ndugu yao huyo alichukuliwa na
mke wa mtoto wa dada yao waliyemtaja kwa jina la Doreen kutoka Songea
mkoani Ruvuma Januari, mwaka huu bila kuwataarifu ndugu, jambo
lililowafanya wamfuatilie na kugundua alipelekwa kwenye kanisa hilo kwa
madai ya kufanyiwa maombi.
Dada wa Galus, Piencia Focus akiwa kanisani hapo
Dada huyo
alisema kuwa aliamua kumtafuta ndugu yake hasa baada ya kupata taarifa
kuwa aliko amekuwa akishinda huku amefungwa mnyororo mguuni, hali
inayomfanya ajisaidie na kula papohapo.
“Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro,” alisema Piencia Focus.
“Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro,” alisema Piencia Focus.
Kaka wa Galus,Peter Focus akizungumza na waandishi wa habari.
Naye kaka
wa Galus, aliyejitambulisha kwa jina la Peter alisema baada ya kupata
taarifa kwamba mdogo wake yupo kwenye kanisa hilo aliamua kufika kwa
ajili ya kumchukuwa kistaarabu lakini cha kushangaza alijikuta
akiangukia kwenye mikono ya waumini hao wakidai yeye ni gaidi na
wakamkwapulia fedha zake.
Peter
alisema alipoachiwa alikimbilia Kituo cha Polisi Wazo Hill ambapo
alifungua jalada lenye Namba za Kumbukumbu WH/RB/6364/14 WIZI TOKA
MAUNGONI.
Waumini wa kanisa hilo wakijibizana na ndugu wa Galus kanisani hapo.
Peter
alisema alilazimika kuungana na dada yake kwa kushirikisha na vyombo vya
usalama ambapo walifika kanisani hapo kwa mara nyingine ili kumkomboa
ndugu yao na kuwatia mikononi waumini waliomwibia fedha zake.
Waandishi
wetu waliokuwa karibu na eneo hilo walizinyaka taarifa hizo na kufika
kanisani hapo ambapo waliwashuhudia ndugu hao wakiwa na polisi
wakimchukuwa mmoja wa watuhumiwa waliodaiwa kumshambulia Peter na
kuondoka naye.
Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship kwa muonekano wa mbele.
Hata
hivyo, jambo la kushangaza ni kitendo cha polisi hao kumwacha Galus
akiwa bado amefungwa kwenye nguzo na mnyororo kanisani hapo wakidai
watamfuata baada ya kumpeleka mtuhumiwa wa unyang’anyi kituoni, jambo
ambalo halikuwa la kweli kwani hawakufika kwa siku hiyo.
Waandishi
wetu walishuhudia timbwili la aina yake kanisani hapo kati ya waumini
wa kanisa hilo na ndugu wa Galus waliorejea kwa lengo la kumchukuwa
ndugu yao baada ya awali kumpeleka kituoni mtuhumiwa wa kumshambulia
Peter.
Waandishi
wetu walipoomba kuzungumza na uongozi wa kanisa hilo ilishindikana na
kujikuta wakishambuliwa kwa maneno huku wakitakiwa kuondoka mara moja
katika eneo la kanisa hilo.
USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA
0 comments:
Post a Comment