Mtayarishaji wa muziki kutoka Combination Sound, Man Walter aliwahi
kutangaza kumaliza tofauti kati yake na 20 Percent aliyewahi kufanya
vizuri kupitia mikono yake na kwa pamoja wakaeleza mpango wa kufanya
mradi mpya.
Man Water ameongea na tovuti ya Times Fm na kueleza walipofikia baada ya ukimya wa muda mrefu tangu walipotangaza hatua hiyo.
“Off Course kwa sasa siwezi kuongelea sana kwa sababu wazo lilienda
vizuri lakini nadhani kuna vitu viwili vitatu vilikwama, sijapata tena
mawasiliano mazuri na 20. Labda tuvute subira tu, kwa sababu kama watu
wana lengo la kufanya jema litakuwa tu…nadhani tuvute subira kwake.” Man
Walter ameiambia tovuti ya Times Fm.
Amefafanua kuwa milango iko wazi kwa 20 Percent kufanya kazi kwake
kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara lakini pia anasubiri sana kufanya kazi
na msanii huyo ili kuwahakikishia watu kuwa hakuna tatizo lolote kati
yao.
20 Percent aliwahi kuchukua tuzo 5 katika kinyang’anyiro cha KTMA kwa kazi alizofanya na Man Walter.
Man Walter ameachia wimbo mpya hivi karibuni aliofanya mwenyewe kwa kushirikiana na Mbatizaji. Unaitwa ‘Wife Material’.
Saturday, September 20, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Man Walter aeleza walipofikia katika kufanya kazi na 20 Percent
0 comments:
Post a Comment