Mamlaka nchini Uturuki zimefunga baadhi ya
mipaka yake na nchi ya Syria kwa mara nyingine baada ya takriban watu
elfu sabini jamii ya kikurdi kutoka nchini Syria kuingia uturuki
wakiwakimbia wanamgambo wa Islamic State.
Siku ya jumapili kulikua
na mapigano kati ya vikosi vya usalama na wapiganaji wa kikurdi
walikuwa wamekusanyika katika eneo la mpaka wakiwatafuta ndugu zao
miongoni mwa wakimbizi.Jamii nyingine ya kikurdi ilijaribu kuvuka hadi nchini Syria ili kujiunga kupambana na wanamgambo ambao wanaelezwa kuwa wamejisogeza karibu na mji wa Kobani.
0 comments:
Post a Comment