Nahodha na mshambuliaji wa klabu Man Utd, Wayne Mark Rooney
ameonyesha kuwa na matarajio ya kufanya vizuri msimu huu licha ya
kukabiliwa na mwenendo mbovu wa kuanza ligi kuu ya soka nchini
Uingereza
chini ya meneja kutoka nchini Uholanzi Louis van Gaal.
Rooney, ametoa msisitizo huo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa
kijamii wa Facebook, ambapo ameandika ana mtazamo tofauti na jinsi
ambavyo watu wanavyo wachukulia Man Utd, kutokana na matokeo mabaya ya
mwishoni mwa juma lililopita baada ya kufungwa na klabu ya Leicester
City mabao 5-3.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameongeza kuwa kila
anapowangalia wachezaji waliopo kwenye chumba cha kubadilishia nguo,
anaona vipaji ambavyo vikichanganywa na umakini wa meneja wao hana
shaka kwamba klabu hiyo itapata mafanikio.
Man Utd, imekuwa haifanyi vizuri tangu mwanzoni mwa msimu huu na
mpaka sasa imeshapoteza michezo miwili, kutoka sare mara mbili na
kushinda mmoja.
Wednesday, September 24, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Rooney Aonyesha Ushupavu Na Kurejesha Salamu Kwa Maadui Wa Man Utd
0 comments:
Post a Comment