Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini humo, Feza
alisema mama yake aitwaye Rose Kessy alikutwa na masaibu hayo mchana wa
saa nane, Jumatano iliyopita akiwa hatua chache kutoka nyumbani kwake,
eneo la Boma ya Siara, Moshono. “Watu wawili wakiwa na pikipiki walimsimamisha akiwa garini anarejea nyumbani, wakamteremsha na kuanza kumsachi, wakachukua pochi yake ambayo ilikuwa na shilingi laki tatu ndani. Wakati wanafanya tukio hilo watu walikuwa wanatazama tu bila kufanya lolote.
“Watu wengine walipita na gari wakataka kusimama, lakini wakaonyeshwa
bastola na kupewa ishara ya kuendelea na safari. Yaani walikuwa
wanafanya wakiwa hawana wasiwasi utafikiri ni askari vile, hivi hapa
ndiyo nimerudi kutoka polisi,” alisema mshiriki huyo ambaye pia aliwahi
kushiriki shindano la Miss Tanzania miaka ya nyuma.
0 comments:
Post a Comment