Search This Blog

Wednesday, September 10, 2014

HABARI PICHAZ: KIBONDE, GARDNER KIZIMBANI TENA!

Watangazaji Ephraim Kibonde (wa pili kushoto) na mwenzake Gardner Habash (wa tatu kulia) wakielekea kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar. (Picha na Maktaba)
WATANGAZAJI Ephraim Kibonde wa Clouds FM na mwenzake, Gardner Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani tena katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar kwa kusababisha ajali, kutotii amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Mkimbu Ramadhan mbele ya Hakimu Aniseta Wambura. 

Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, Dar ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Oktoba 2, mwaka huu itakapotajwa tena.

0 comments:

Post a Comment