Mshambuliaji
wa klabu ya PSG na timu ya taifa Ya Sweden Zlatan Imbrahimovic ameweka
rekodi mpya na ya kipekee ya kuwa mfungaji bora wa wakati wote nchini
Sweden baada ya kuifungia nchi yake mabao mawili katika mchezo wa
kirafiki wa
kimataifa dhidi ya Estonia.Rekodi hii ni yakuwa na magoli 50 kwenye mechi za kimataifa 99 alizocheza Zlatan. Aliyekuwa ameshikilia rekodi hii toka mwaka 1932 ni Sven Rydell mwenye magoli 49 kutoka kwenye mechi 43.
0 comments:
Post a Comment