Search This Blog

Wednesday, September 10, 2014

TAHADHARI MUHIMU: MADEREVA WA BODABODA WANAVYOIBIWA KIRAHISI PIKIPIKI ZAO!

TUMEKUWA tukiandika mbinu mbalimbali ambazo matapeli huzitumia ili kujipatia fedha au mali kwa njia ya udanganyifu. Matapeli hao hutumia ujanja kuwaibia watu fedha au
mali na wakati mwingine mwenye mali hutoa kwa hiari yake akiamini kuwa aliyekuwa naye ni mtu mzuri.

Leo tunawaangalia wenye mali au madereva wa pikipiki wanavyoibiwa kiulaini yaani kirahisi na matapeli au wezi sehemu mbalimbali.Kuna mbinu nyingi sana ambazo wezi wa pikipiki au jina maarufu bodaboda hutumia kufanikisha malengo yao hayo mabaya ya wizi.


Nikupe simulizi ya dereva mmoja wa bodaboda alivyoibiwa hivi karibuni baada ya kutoa ufunguo wa chombo chake hicho kwa hiari yake.Siku hiyo aliamka mapema asubuhi akijua kwamba anakwenda kufanya kazi ya kujiingizia riziki ili fungu moja ampelekee tajiri yake naye apate chochote cha kuendeshea maisha yake. 

Alipofika maeneo ya Ilala, jijini Dar es Salaam alikutana na ‘abiria’ ambaye alionekana ni mtanashati na mazungumzo yao yakawa hivi:

Mteja: Haloo hujambo?
Dereva wa bodaboda: Sijambo kaka, shikamoo!
Mteja: Marahaba. Nina shida ya usafiri.
Dereva wa bodaboda: Unakwenda wapi?

Mteja: Nina mzigo wangu nataka kwenda kuuchukua kanisani.
Dereva wa bodaboda: Kanisa gani?
Mteja: St Joseph, kamzigo kadogo tu.

Dereva wa bodaboda: Sawa, ukishachukua mzigo unaupeleka wapi?
Mteja: Ni wewe utakayeuleta nyumbani kwangu.
Dereva wa bodaboda: Sawa.

Mteja yule alimuelekeza dereva yule wa bodaboda hadi kwenye mtaa mmoja maeneo ya Ilala. Alimuamuru dereva wa pikipiki kusimama kando ya nyumba moja ambayo ina wapangaji lakini ni ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Baada ya kufika katika nyumba hiyo mtu huyo aliingia ndani na kumuacha dereva wa bodaboda akiwa nje. Alikaa pale kwa dakika kama mbili au tatu hivi baadaye alikuja kwa dereva.
Mteja: Hapa ni nyumbani kwangu, ule mzigo nikiupakia kule kanisani utauleta katika nyumba hii.
Dereva wa bodaboda: Nikija hapa niulize nani? Si bora ungenionesha mtu wa kuupokea?
Mteja: Wewe mbona una kiherehere? Hapa ni nyumbani kwangu watu wote hapa ni wa familia yangu. Utakayemkuta yeyote ukimpa ataupokea,  kwa sababu mzigo wenyewe ni vitabu vya dini ambavyo nataka kuvipeleka huko Masasi, Ndanda Misheni.
Dereva wa bodaboda: Kwani wewe ni mtu wa kule Ndanda?
Mteja: Ni mwenyeji wa mitaa ya kulekule sehemu moja inaitwa Mtandi Misheni. Siyo mbali kutoka pale Ndanda Misheni na wewe je?
Dereva wa bodaboda: Mimi pia wa kulekule natokea sehemu moja inayoitwa Mangaka, sasa hivi ni Makao Makuu ya Wilaya Mpya ya Nanyumbu.
Mteja: Basi imekuwa vizuri, kumbe nimempata mtu wa nyumbani kabisa. Basi twende kuchukua vitabu.
Safari ilianza kutoka Ilala akapitia Mtaa wa Uhuru, akafika kwenye kona ya Uhuru na Msimbazi na kufika katika kanisa la St Joseph. Alimuambia mwenye bodaboda aingie ndani, akaingia.
Baada ya kuingia alimuacha dereva wa bodaboda sehemu na pikipiki yake, yule mteja alizunguka nyuma ya kanisa na alikaa huko kwa dakika kadhaa. Baadaye alijitokea na akazungumza na mwenye bodaboda.
Mteja: Huyu mzungu hapa noma kweli.
Dereva wa bodaboda: Kwani kafanyeje?
Mteja: Kakataa wewe kwenda kuchukua vitabu kasema eti nikavipakie mimi!

0 comments:

Post a Comment