1.
Kama ulitozwa faini barabarani mwaka jana au mwaka huu basi ujue
mkwanja wako ni sehemu ya hii hesabu mpya……….. unaambiwa faini
zinazotozwa na askari wa usalama
barabarani zinaiingizia serikali
mabilioni, makusanyo yake kwa mwaka 2013 pekee ni Bilioni 16 lakini ya
mwaka huu ndio imetisha zaidi kwa sababu kuanzia January mpaka June ni
Bilioni 19 zimekusanywa.
Matrafiki wadai kutakiwa kupeleka Milioni 15 kila mwezi. #HabariLEO
2.
Unaambiwa ile stori nyingine kubwa ya Tanzania kuhusu sarafu mpya
Tanzania ambayo itakua ya shilingi mia tano, imetambulishwa na itaanza
kutumika mwezi ujao ikiwa na sura ya Karume ambapo noti ya shilingi mia
tano itaanza kuondolewa taratibu kwa mujibu wa gazeti la #HabariLEO
3.
Stori namba 3 ni kutoka sehemu inaitwa Simiyu ambako Polisi
wamewakamata watu wanne ambao wamekutwa shamani wakilima uchi ishu
ambayo inahusishwa na imani za kishirikina.
4.
Wafanyakazi wa TTCL wanaidai kampuni yao malimbikizo ya mshahara ambayo
ni Bilioni 7.8 kwa miaka saba sasa, Mwajiri atakiwa kuwalipa mara moja.
#HabariLEO
5. Namba 5 kwenye hii post ni stori iliyoandikwa na gazeti la #Jangwani likisema Jerry Muro ndio afisa habari mpya wa Yanga.
Monday, September 8, 2014
Home »
» Sentensi 5 zenye stori za Magazeti ya Tanzania leo Sept 8.
0 comments:
Post a Comment