Search This Blog

Friday, September 12, 2014

NEW UPDATES: PICHA NA TAARIFA ZAIDI KUHUSU AJALI YA MABASI YA SUPER FEO NA UPENDO LEO!

Ajali mbaya imetokea asubuhi hii ikihusisha mabasi mawili ya kampuni ya SUPER FEO likitokea Dodoma kuelekea Songea na basi la UPENDO TRAVELLERS kutokea Dodoma kuelekea jijini Mbeya.


Taarifa za kutoka eneo la tukio zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni punde aliyekatisha barabarani na  mwendo kasi wa basi la upendo bila umakini wa dereva wa basi hilo. 

Walisema abiria waliokuwa katika basi la upendo kuwa walikuwa wakilifuata basi la Super feo kwa kasi bila kuacha safety distance (nafasi ya usalama kati ya basi moja na lingine nyuma au mbele ) hali iliyopelekea ajali hiyo kutokea pale dereva wa basi la Super feo aliposimama ghafla kuepuka kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani.

Taarifa zinaendelea kudai kuwa dereva wa basi la upendo amevunjika miguu na wengine wamejeruhiwa vibaya!
KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU AJALI HII TUTAENDELEA KUWAJUZA!



0 comments:

Post a Comment