Search This Blog

Friday, September 12, 2014

'Hanuman' atumiwa kitambulisho

Maafisa wa utawala nchini India, wanachunguza ambavyo kitambulisho cha elektroniki kimetengezwa kikiwa na picha ya Hanuman mungu wa kihidni na kutumwa kupitia kwa posta.
Kitambulisho hicho kina picha ya mtu anayejulikana kama Hanuman kutoka kwa kipindi kilichojuolikana kama Ramayana, akiwa amevalia mikufu ya dhahabu na taji la kifalme.
Kitambulisho chenyewe kilipatikana wakati mfanyakazi wa posta alijaribu kuifikisha kwa mtu aliyetumiwa ila hangeweza kupata anwani ya mtu yeyote anayejulikana kama Hanuman.
Alipoangalia kwa picha , aligundua kuwa huenda ilikuwa mchezo wa danganya toto. Bado haijaulikana ni nani aliyeweka alama ya kidole kwenye kadi hiyo.
Hanuman alijulikana kama mtoto wa mungu wa kihindi aliyejulikana kama Pawan, na kadi yenyewe ina namba ya simu na anwani ya sehemu iliyo katika jimbo la Rajasthan.

Hanuman alijulikana kama mungu wa kihindi mwenye nguvu za ajabu na mtiifu sana
Kwa kawaida Hanuman huonekana akiwa na uso wa Nyani pamoja na mkia. Kuna hekaya za kale kuhusu Hanuman kote nchini India.
Mfanyakazi huyo wa posta Heeralal Saini, aliyeipokea kadi hiyo ili aweze kuifikisha kwa mtu aliyetumiwa, aliirejesha kwenye kituo cha posta baada ya kukosa kumpata mtu kwa jina hanuman.
'Hanuman ni nani?'
Hanuman ni mmoja wa miungu wanaobudiwa na watu nchini India na pia kuna hekaya nyingi tu kwenye vitabu vya kihindi kumhusu. Huonekana kama binadamu mwenye uso wa Nyani na mkia mrefu.
Mara kwa Mara yeye husemekana kuwa mtoto wa mungu mwingine wa kihindi Pawan na anasifika kwa kuwa mtiifu na mwaminifu pamoja na kuwa na nguvu za ajabu.

0 comments:

Post a Comment