Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
STAA wa filamu Bongo, Ruth
Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vilivyokuwa vimeuteka
ujana wake ni pamoja na matumizi ya mkorogo (kitaulo) ambapo ilikuwa vigumu kuacha
baada ya kuokoka.
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema kutokana na starehe za
ujana pamoja na kutaka kuonekana mrembo, alitumia vipodozi hatari bila
kujua kwamba vina madhara makubwa mwilini mwake.
“Kusema kweli niliamini mkorogo ni kitu ambacho kingeniongezea mvuto kwa kiasi kikubwa, bila kujua kuwa nilikuwa najisababishia madhara mwilini.
Pia nilikuwa nafanya kitu kisichompendeza Mungu, katika kujitakasa na maovu yangu kwa Bwana ndiyo maana nikaamua kuacha kabisa kujichubua japo haikuwa rahisi,”alisema Mainda.
0 comments:
Post a Comment