![](http://3.bp.blogspot.com/-2GU7auaiQaw/VBJ53xQvQLI/AAAAAAAAmcM/XgV7CaNxAuQ/s400/sitta.jpg)
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta
BUNGE Maalum la Katiba linaloendelea na vikao vyake
mjini Dodoma, halitaendelea baada ya Oktoba 4, mwaka huu hadi baada ya
uchaguzi mkuu mwakani, hali inayoelezwa kuwapa ulaji wa bure wajumbe
wake kwa vile katiba mpya haitapatikana kwa sasa.
Kikao maalum kati ya Rais Jakaya Kikwete
na viongozi wa Kituo cha Demokratia Tanzania (TCD) kilikubaliana kwamba
muda uliobaki hauwezi kumaliza mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya,
hivyo suala hilo lisubiri hadi baada ya uchaguzi mkuu utakaompata rais
mpya atakayeamua kama suala hilo liendelee au lisiendelee.
Mara baada ya kususia kwa wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) katika vikao hivyo, wito kutoka makundi mbalimbali ya
kijamii umekuwa ukitolewa kuwataka kurejea ili kunusuru mchakato huo,
lakini wamebakia na msimamo wao wakisisitiza kuwa Katiba Mpya haiwezi
kupatikana pasipo maridhiano ya kitaifa.
0 comments:
Post a Comment