Search This Blog

Tuesday, September 16, 2014

Wafanyakazi wa kigeni watimuliwa Sudan:K

Serikali ya Sudan kusini imeagiza wafanyakazi wa kigeni wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na kampuni za kibinafsi waondoke nchini kufikia katikati ya mwezi Oktoba.
Wizara ya leba imesema kuwa hatua hiyo inalenga kubuni ajira kwa raia wa Sudan Kusini.

Mashirika yalioathiriwa na tangazo hilo yametakiwa kutangaza nyadhifa zilizo wakati wa kukamilika kwa muda huo wa mwisho.
Mashirika yaliyoathirika yametakiwa kutangaza nafasi za kazi pindi nafasi hizo zitakapofungwa.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya leba, inasema kuwa nafasi za kazi zilizokuwa zinashikiliwa na wafanyakazi wa kigeni, lazima zichukuliwe na raia wa Sudan Kusini.
Wala wanaotakiwa kufuata masharti hayo ni mashirika ya kutoa misaada na makampuni binfasi.
Hata hivyo, wizara ya leba inasema sharti hili litaathiri tu nafasi kubwa kubwa katika mashirika hayo kama vile nafasi za wakurugenzi wakuu, wasimamizi na maafisa wa uhusiano mwema.
Hatua hii huenda pia ikaathiri maelfu ya wafanyakazi wa kigeni.
Inakuja wakati muhimu huku Sudan Kusini ikiwa bado inakabiliana na athari za vita vilivyozuka mjini Juba mwezi Disemba mwaka 2013, kufuatia mapambano kati ya Rais Kiir na aliyekuwa naibu wake Riek Machar.
Mashirika ya misaada yameonya kuwa nchi hiyo iko katika hali ya hatari na huenda ikakabiliwa na uhaba wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Shirika la misaada la Uingereza, linasema kuwa ikiwa amri hiyo itatakelezwa huenda ikaathiri sana mpango wa misaada kwa maelfu wanaouhitaji.

0 comments:

Post a Comment