Search This Blog

Saturday, September 13, 2014

SAD NEWS: MTU MMOJA AFARIKI SERENGETI FIESTA SHINYANGA USIKU WA KUAMKIA LEO!


Mwili wa marehemu Musa Shija mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa mtaa wa Mwalugoye kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga aliyeuawa kwa kushambuliwa akiwa kwenye Fiesta usiku wa kuamkia leo katika uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa wa

Shinyanga.

Akizungumza mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema uchunguzi wa kitaalam walioufanya unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa na kitu butu kichwani na kusababisha kuvuja damu kichwani kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa kijana huyo aliuawa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana nje ya fensi la uwanja mdogo wa Kambarage palipokuwa panafanyika tamasha la Fiesta.

Hata hivyo amesema jeshi la polisi litatoa taarifa kamili baadaye kwani linaendelea kufanya uchunguzi
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA NDANI YA UWANJA MDOGO WA KAMBARAGE UMATI HUU WA WATU WAKISELEBUKA PASIKUJUA YAJAYO.

0 comments:

Post a Comment