Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamuru mabango ya hekeheka za
uchaguzi yenye nembo ya kauli mbiu ya 'Bring Back Jonathan 2015'
yang'olewe mara moja.Mabango hayo yamelaaniwa vikali kwenye mitandao ya kijamii kwani
yanaonekana kuiga kauli mbiu iliyotumiwa katika kampeini ya kuitaka
serikali kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram
mwezi Aprili mwaka huu.
Kundi hilo la wapiganaji wa kiisilamu
bado linawashikilia wasichana hao, Wakati ambapo mabango ya Bring Back
Jonathan 2015 yaliowekwa kando ya barabara kuu mjini Abuja, yalilaaniwan
vikali nchini Nigeria na
kimataifa kupitia katika mitandao ya kijamii.
Watu
walihisi kuwa ilikuwa ni kama kejeli kwa kampeini ya 'Bring Back Our
Girls' ambayo ilienea kote duniani baada ya Boko Haram kuwateka nyara
wasichana wa shule ya Chibok.
Wasichana hao 219, bado hawajulikani waliko miezi mitano baada ya kutekwa kwao.
Rais Jonathan, ameyataka mabango hayo kuondolewa kwenye barabara za mji haraka iwezekanavyo.
Katika
taarifa yake alisema yeye pamoja na wanigeria wengi wanahisi kuwa
kampeini hiyo ilikuwa na nia mbaya na kusisitiza kuwa juhudi bado
zinafanywa kuwoakoa wasichana hao waliotekwa na Boko Haram.
Wednesday, September 10, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Rais Jonathan - mabango yang'olewe
0 comments:
Post a Comment