Ripota
wa TZA nchini Uganda Bill the African ameripoti kuhusu hii ya vurugu
kubwa kutokea kwenye mpaka wa Uganda na Sudan eneo la Ufoju kutokana na
raia wa nchi hizi mbili kutoafikiana kwenye baadhi ya mambo ambapo pia
baadhi ya viongozi wa Uganda kwenye eneo hilo walikamatwa na Polisi wa
Sudan.
Kikubwa kinachosababisha vurugu hizi ni mipaka ya hizi nchi kushindwa
kujulikana kila mmoja anatakiwa kuishia wapi ambapo pia Waganda ambao
wamekua wakiingia Sudan wamekua wakikamatwa na Polisi wa Sudan na kupewa
mateso makubwa.
Jeshi
la Polisi Uganda limesema kwamba katika vurugu hizi karibu nyumba 15 za
raia wa Sudan wanaoishi Uganda zimechomwa moto likiwemo kanisa la
kipentekoste linalodaiwa kuwa la raia wa Sudan.
Wednesday, September 17, 2014
Home »
Maxwellpain.blogspot.com
» Picha 5 za kilichotokea kwenye mpaka wa Sudan na Uganda. #vurugu
0 comments:
Post a Comment