Search This Blog

Friday, September 12, 2014

MJUE KWA UNDANI JAJI MWANAMKE ANAYETOA HUKUMU YA OSCAR PISTORIUS!

JAJI Thokozile Matilda Masipa mwenye umri wa miaka 66, alizaliwa Oktoba 15, 1947 Soweto nchini Afrika Kusini na wakati mmoja aliajiriwa kama karani na mpishi wa chai.



Jaji Thokozile Matilda Masipa akisoma hukumu ya Pistorius.
Kuna kipindi nusura aachane na masomo yake kwa kuwa alidhani hatafanikiwa kwa vyovyote vile licha ya masomo aliyokuwa anachukua. 

Lakini mama yake aliendelea kumpa motisha ya kuendelea na masomo yake. Alikwenda chuo kikuu na baada ya kumaliza aliajiriwa kama mwandishi wa habari kabla ya kufungwa jela wakati ya vita vya ukombozi.

Oscar Pistorius akiwa Mahakama Kuu kusikiliza hukumu yake jana.
Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, Jaji Masipa alirejea tena chuo kikuu ambako alisomea uanasheria, wakati huo Afrika Kusini ilikuwa imeanza kuzingatia utawala wa demokrasia.
Aliteuliwa kuwa jaji mwaka 1998 na kuwa Mwafrika wa pili wa kike kuteuliwa jaji nchini Afrika Kusini.

Lakini tangu kesi ya Pistorious kuanza, wengi wamekuwa wakichunguza hukumu ambazo amezitoa kati kesi zilizopita.
Mwaka 2009, alimhukumu ofisa mmoja wa polisi kifungo cha maisha gerezani baada ya kumpata na hatia ya kumuua mke wake wa zamani. Alisema hakuna aliye juu ya sheria na kuwa ofisa huyo anastahili kwenda jela kwa kushindwa kutii sheria. 

Mwaka jana alimhukumu mwanamme mmoja miaka 252 gerezani baada ya kumpata na hatia ya kuwabaka wanawake watatu katika makazi yao.

Jaji Thokozile akiwa kazini.
Akiwa mahakamani, ambako amekuwa akisikiliza kesi ya mwanariadha mlemavu Oscar Pistorious tangu mwezi Machi, Jaji Thokozile Masipa amekuwa akionekana kama mtu ambaye fikra zake ziko mbali, mtulivu na mtu anayetazama mambo kwa undani.
Akiwa amevalia miwani, jaji huyu hajizuii kuzungumza mengi na mara nyingi hutabasamu tu. Tangu mwanzo wa kesi hii, wakosoaji wake ambao wengi ni wanaume, wamekuwa wakinadi kuwa kujitenga kwake ni ishara kuwa hana ufahamu wa kutosha au kutishwa na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikitangaza vikao vya kesi hiyo moja kwa moja. 
Wakili mmoja nchini Afrika Kusini Jeremy Gauntlett alinukuliwa akisema kuwa Jaji Masipa ana wasiwasi mwingi kutokana na kuwepo kwa waandishi wa habari mahakamani.

Huku kesi hii ikimalizika, utulivu wa Jaji Masipa, ukilinganisha na vilio na sarakasi zilizokuwa mahakamani kutoka kwa watu waliokuwa wakilia mara kwa mara wengi wao wanaume wazungu, Jaji Masipa amepata sifa nyingi na heshima ya hali ya juu. 

Alijiepusha kuingilia kati mawakili walipokuwa wakiwasilisha ushahidi au wakati walipokuwa wakiwahoji mashahidi na mshitakiwa, lakini kila alipoingilia wengi walifurahiswa na umakini na usawa ambao alikuwa akiuonyesha kwa pande zote. 

Jaji huyo ni mmoja wa watu waliopata wakati mgumu sana wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi na miongoni mwa wale waliotambua kuwa maisha siyo kazi unayofanya au malengo maishani bali ni kufanya taifa lako kuwa zuri alisema jaji mmoja wa mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini, Albie Sachs.

0 comments:

Post a Comment