Mahakama ya rufaa nchini India imezuia mpango wa jimbo la Kerala Kusini mwa nchi hiyo kupiga marufuku pombe.
Mamia
ya wamiliki wa baa walikuwa wamepinga marufuku hiyo ambayo ingeanza
kutekelezwa Ijumaa hiikwa kusema kuwa itaporomosha utalii.
Hoteli za kifahari zingeponea marufuku hiyo na mahakama iliamua kuwa marufuku hiyo haina msingi.
Jimbo la Kerala ndilo lenye kiwango kikubwa zaidi cha walevi nchini India.
Uamuzi wa mwisho kuhusu swala hilo, utatolewa na mahakama kuu.
0 comments:
Post a Comment