Search This Blog

Monday, September 8, 2014

HATIMAYE NAY WA MITEGO AMWANIKA MTOTO WAKE NA SKAINA WA BONGO MOVIE!

Mambo hadharani! Baada ya kimya kirefu, staa wa Hip hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mara ya kwanza amemwanika mtoto aliyezaa na msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ na kukiri kwamba ni wa kwake.

Mtoto wa staa wa Hip hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.
Akizungumza nasi, Nay alisema kuwa anampenda mwanaye huyo na kwa sasa anaishi naye nyumbani kwake. Kimara-Baruti, Dar na ana umri wa miaka miwili na nusu anayejulikana kwa jina la Munie.
Mama mzazi wa Munie ambaye ni msanii wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ akipozi.
“Nampenda sana mwanangu ndiyo maana nimeamua kumchukua kwa mama yake Skaina na kuja kumlea kwangu, analelewa vizuri sana na mama yake ambaye ni Siwema namshukuru Mungu mwanangu anaendelea kukua, nafurahia sana kukaa na mwanangu karibu tofauti na alivyokuwa kwa mama yake,” alisema Nay wa Mitego.
‘Nay wa Mitego’ akiwa na mwanaye.
Skaina aliwahi kukiri kuwa mwanaye huyo baba yake ni Nay lakini baada ya Nay kuulizwa alichengachenga hivyo sasa ameamua kumuweka wazi.

0 comments:

Post a Comment