Nafasi
yake nyingine kubwa ya kuzungumziwa toka ameanza muziki ni hii
aliyoipata baada ya kufanya wimbo wa ‘Ole Themba’ na kundi maarufu la
Uhuru South Africa.
Ni
kolabo ambayo mpaka August 31 2014 usiku video yake YouTube ilikua
imebakiza sio chini ya views elfu mbili ili kufikisha views laki moja za
wote walioitazama toka iweke July 2014.
Yafuatayo ni mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’.
1.
Video hii ya ‘Ole Themba’ imeanza kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya TV
Africa ikiwemo MTV Base pamoja na TV ya Ufaransa ya TRACE Urban ambao
tayari wameshamtumia Linah mkataba wa makubaliano.
2.
Wakati aliposafiri kwenda Afrika Kusini kuirekodi hii single na Uhuru,
alikaa kwa mwezi mmoja bila kufanya chochote mpaka kufikia kukata tamaa
manake Uhuru kama walimuwekea ‘pozi’ japokua Linah alikua na pesa
mkononi tena milioni za Tanzania kwa ajili ya kulipia kurekodi nao hiyo
single kama makubaliano yalivyokuwa.
3.
Linah anasema Producer wa Uhuru aliwatajia hela nyingi kurekodi hiyo
kolabo akidhani watashindwa kuilipia lakini haikua hivyo, mwanzoni
aliwawekea pozi kwa kuagiza atumiwe link za video za Linah YouTube ili
ajue uwezo wake lakini hakuwahi kuzitazama.
4.
Producer huyu alikua akipigiwa simu mara nyingi lakini hakuwa anapokea
na hata msg anaweza kujibu au kutojibu ambapo linah anasema ‘ilikua
ngumu sana mwanzoni lakini baada tu ya kuingia studio kuweka voco ya
kwanza nikapata na kolabo hapohapo, yani walikubali uwezo wangu’
5.
Baada ya Uhuru kuona single ya ‘Ole Themba’ imeanza kuwa kubwa kwa
kufanya vizuri kwenye Radio na TV kulitokea kama kutokuelewana kidogo
kwa kuona Linah anaanza kupata hela.
6.
‘Waliitengeneza kama na wao wana haki na wimbo wenyewe lakini uzuri ni
kwamba tulishasaini mkataba mwanzoni kuwa wimbo wametuuzia ni mali yetu
na wala hawana haki yoyote, alietunga melody alisaini na tumemlipa so
hausiki tena, tulimlipa kila mtu na kazi yake…. namshukuru Mungu iliisha
vizuri’- Linah
Monday, September 1, 2014
Home »
» #Exclusive: Mambo 6 ya kufahamu kuhusu Linah na hit single ya ‘Ole Themba’
0 comments:
Post a Comment