Watu
wawili wamefariki dunia baada ya ajali iliyolihusisha gari aina ya
Mitsubishi Canter lililosajiliwa kwa namba T. 497 AFR lililokuwa
likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Sefania Msigalamwenye
miaka 40 ambaye ni mkazi wa Madabaga mkoani hapa.
Taarifa
kutoka kwa maafisa wa polisi mkoani Mbeya zinaeleza kuwa ajali hiyo
imetokea baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka alfajiri ya kuamkia
leo majira ya saa 10:15 katika mteremko mkali kijijini Itewe, wilaya ya
Mbeya vijijini mkoani hapa na kisha kusababisha kifo cha Dereva wa gari
hilo Sefania Msigala na abiria wake Riziki Mhanga mwenye miaka 45 mkazi
wa Njombe.
Chanzo
cha ajali hiyo bado hakijafahamika ingawa bado kinachunguzwa huku miili
ya marehemu ikihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
0 comments:
Post a Comment