Search This Blog

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, September 24, 2014

Sababu za Madee kushikiliwa na Polisi.. chanzo ni hiki cha jamaa wawili wa Pikipiki

jpsTaarifa zimethibitishwa kuhusu staa wa hit single kama ‘pombe yangu’ ‘tema mate tuwachape’ na ‘ni shidaah’ Madee ambae ni msanii kutoka kundi la TipTop Connection kushikiliwa na Polisi.
Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo ambae ni Babtale
, Gossip Cop Soudy Brown kwenye You heard inayosikika kupitia XXL ya CloudsFM J3-Ijumaa alisema ‘inasemekana Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni’
Babtale alipoulizwa akasema ‘Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora kwa hiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki alafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma, pikipiki ilivyodondoka yule aliekua nyuma kwenye pikipiki ambae ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliekua anaendesha hiyo pikipiki’
Madee 1‘Wakamchukua na kwenda nae maskani Tiptop… mama yake akaja akasema msipeleke Polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu, Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake…… saa nne asubuhi yule mama akaja na Polisi badala ya kuja na mwizi mwenzake akaja na Polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop, walimchukua huyo Muhalifu kwenye Land rover mpaka Polisi Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa’
‘Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka Hospitali, nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa Polisi akaripoti…. kufika kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka Hospitali akawaambia huyu ni mwizi ameiba, ikabidi Dogo aingizwe ndani jana akalala pale Polisi Magomeni’
note 3‘Asubuhi yake Madee akaenda kituoni kama kufata Mwalifu wake na kutaka simu yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe Kigamboni…. saa kumi na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia msg anasema Madee analalamika mbona humfatilii nikauliza kuna nini tena akasema wamemuingiza ndani, nikapiga simu Polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako tulitaka kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu, nikapiga simu kwenye vyanzo vyangu vya msaada tukamtolea dhamana…. ni hilo

  USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA  KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI PIGA NO. 0712473752

Risasi alizopigwa jamaa alietaka kumuua Mbunge kwa panga.

short gunWakati Mbunge Steven Ngare akikagua mradi wa maendeleo kwenye shule ya msingi huko Kenya kuna jamaa alijitokeza na kujaribu kutaka kumvamia ili amkatekate kwa panga lakini kabla hajamfikia tayari mlinzi wa mbunge akawa amemuona.

Imetokea kwenye kijiji cha Kariti kaunti ya Kainyaga huko Kenya ambapo baada ya mlinzi kuona na kupata uhakika jamaa huyo alikua na nia mbaya, alichukua bastola yake na kumpiga risasi tatu zilizosababisha mwanaume huyo kufariki papohapo huku sababu zaidi za kwanini alitaka kufanya hivyo zikiwa hazijulikani.
Kwa mujibu wa Citizen TV, mtu huyu alitaka kumshambulia mbunge huyu muda mfupi tu baada ya kumkata kwa panga mwalimu mkuu wa shule hiyo kulikompa majeraha na kumfanya awe mahututi hospitalini hadi sasa.
NYINGINE
Taarifa nyingine kutoka Radio Jambo ya Kenya ni kuhusu hii ya mshukiwa mkuu wa mauaji ya Mbunge aitwae George ambae alifariki baada ya kunywa kinywaji kilichowekewa sumu, amepoteza kwa mara nyingine tena ombi la kutaka kuachiwa kwa dhamana kwa sababu alizozitoa kwamba ana matatizo ya kiafya.
Paul Wainaina ni mmiliki wa Baa ambako inadaiwa marehemu Mbunge George ndiko alikowekea sumu kwenye kinywaji chake.
NYINGINE:
Malipo ya umeme yatapungua nchini Kenya mwezi huu kutokana na kuanzishwa kwa miradi mingi zaidi ya kuzalisha umeme ambapo kampuni husika imesema huenda malipo hayo yakapungua kutoka shilingi 17 za Kenya mpaka shilingi sita kwa kilowati moja ambapo pia serikali ya nchi hiyo inajitahidi kufanikisha mradi wake wa kuongeza megawati elfu 5 za umeme kufikia mwaka 2017.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA  KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USHAURI PIGA NO. 0712473752

Capital One: Hiki ndicho Southampton walichoifanya Arsenal nyumbani kwao jana!

IMG_7518.JPGArsenal walivubja rekodi ya miaka miwili kwenye Barclays Premier League jumamosi iliyopita kwa kukamilisha jumla ya pasi 741 katika ushindi wao wa magoli 3-0 dhidi Aston Villa.
Usiku wa jana katika uwanja wao wa
Emirates ilikuwa zamu ya vijana wa Arsene Wenger kufundishwa soka na vijana wa Ronald Koeman Southampton.
Southampton ambao waliutawala mchezo wa jana kwa kiasi kikubwa walianza kwa kufungwa katika dakika ya 14 kwa goli zuri la adhabu ndogo nje kidogo na eneo la hatari la Southampton.
Saints wakasawazisha kwa mkwaju wa penati kupitia Dusan Tadic.
Katika cha pili beki wa kulia wa kiingereza Nathaniel Clyne alifumua shuti kali la umbali yadi 39 lilomshinda golikipa mpya wa Arsenal David Ospina.
Na mpaka mpira unamalizika Arsenal 1-2 Southampton – na kwa Matokeo hayo Gunners wameyaaga mashindano ya Capital One.
Timu zilipangwa hivi:
Arsenal: Ospina 4; Bellerin 5 (Akpom 86), Chambers 6.5, Hayden 5, Coquelin 5; Rosicky 5, Diaby 5.5 (Cazorla 67); Campbell 5.5 (Oxlade-Chamberlain 71), Wilshere 5, Podolski 4; Sanchez 6.
Subs: Gibbs, Mertesacker, Martinez, Ajayi.
Booked: Rosicky, Wilshere
Manager – Arsene Wenger: 5
Southampton: Forster 6; Clyne 8, Fonte 7, Gardos 7.5, Targett 7 (Bertrand 85); Wanyama 6.5, Schneiderlin 9; Mane 7.5 (Long 72), Davis 7, Tadic 7.5; Pelle 7.
Subs: Davis, Cork, Mayuka, Reed, McCarthy.
Booked: Wanyama, Pelle, Tagett, Forster
Manager – Ronaldo Koeman: 8.
Referee: Keith Stroud.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Torres Afungua Akaunti Akiwa na AC Milan Ya Italia

Mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Fernando Torres ameanza kufanya kazi yake akiwa na klabu ya AC Milan iliyomsajili kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Chelsea ya jijini London nchini Uingereza.
Torres, aliyelazimika kuondoka Chelsea kutokana na changamoto ya upatikanaji wa nafasi katika
kikosi cha kwanza, ameanza kufanya yake akiwa na AC Milan baada ya kufunga bao lake la kwanza usiku wa kuamkia hii leo wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Italia, Sirie A dhidi ya Empoli.
Katika mchezo huo, Torres alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza baada ya kuanzishwa kama mchezaji wa akiba katika mchezo uliopita.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alifunga bao hilo kwa kichwa katika dakika ya 43, kabla ya Keisuke Honda hajafunga bao la kusawazisha katika dakika ya 58.
Mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili na hivyo kuifanya AC Milan kusogea hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya Sirie A kwa kufikisha point Saba.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Big Brother Africa 2014: Picha nzuri za washiriki 6 waliotajwa hivi karibuni akiwemo Mtanzania

Mashabiki wa shindano la Big Brother Africa wanaoisubiria kwa hamu msimu mpya utakaoanza mwezi ujao uliopewa jina la ‘Hot Shots’.
Hivi karibuni wametajwa washiriki wengine sita wanaoziwakilisha nchi zao. Kutoka Tanzania mrembo Irene Laveda ambaye
ana kipaji cha kuigiza anaungana na Idris ambaye ni mpiga picha  kuiwakilisha nchi yetu katika jengo hilo.
Angalia picha za washiriki hao sita waliotajwa hivi karibuni.

Laveda (Tanzania)

M'am Bea (Ghana)

Luis (Namibia)

Lilian (Nigeria)

Kacee Moore (Ghana)

JJ (Zimbabwe)

Dr Dre aongoza orodha ya Forbes ya wasanii wa Hip Hop walioingiza pesa nyingi zaidi 2014, orodha kamili

Dr Dre aongoza orodha ya Forbes ya wasanii wa Hip Hop walioingiza pesa nyingi zaidi 2014, orodha kamili  Daktari wa midundo, Dr Dre ameongoza orodha ya Forbes ‘Hip Hop Cash Kings 2014’ akivaa taji hilo baada ya kuingiza kiasi cha $620 million mwaka huu.
Sio tu kwamba Dr Dre ameongoza orodha hiyo bali ameweka rekodi
ya aina yake kwa kuwa kiwango alichoingiza kinazidi jumla ya fedha zote walizoingiza wasanii wengine 24 walioingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Dre anarudi kwenye nafasi yake hiyo aliyokuwa akiishikilia mwaka 2012 kabla ya kufunikwa na P. Diddy mwaka jana.
Anaongoza orodha hiyo kwa kishindo baada ya kampuni ya Apple kutangaza kuinunua kampuni anayoimiliki kwa kushirikiana na Jimmy Lovine ya Beats Electronics kwa $3 billion.
Nafasi ya pili imeshikiliwa na Jay Z na P.Diddy ambao wamefungana kwa kuingiza kiasi cha $60 million kila mmoja.
Jay Z ameingiza kiasi hicho kupitia matamasha mengi aliyoyafanya, biashara zake na album yake ya Magna Carter Holy Grail iliyofikia mauzo ya Platinum hata kabla haijaachiwa baada ya kampuni ya Sumsang kununua nakala milioni moja.
P. Diddy yeye aliingiza kiasi hicho ($60 million) kupitia biashara zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wake wa mavazi wa Sean Jean, Revolt TV na mengine.

Rapper wa Young Money, Drake anashikilia nafasi ya 4 katika orodha hiyo akiwa ameingiza kiasi cha $33 million. Kiasi hiki kimetokana na mauzo ya album yake ya ‘Nothing Was The Same’ iliyouza nakala zaidi ya Milioni 4 duniani kote. Kiasi kingine kiliigia kupitia endorsement ya Jordan na tour yake.

Nafasi ya 5 imeshikiliwa na wasanii wanaofanya kazi pamoja Macklemore & Ryan Lewis ambao wameingiza kiasi cha $ 32 million. Wasanii hao walifanikiwa mwaka jana kushinda tuzo nne za Grammy kati ya saba walizokuwa wakiwania. Ushindi huo uliwasaidia kupata shows nyingi zaidi na kufanya biashara kubwa mtaani.

Kanye West amekamata nafasi ya 6 akiwa ameingiza kiasi cha $30 million. Tour yake ya ‘Yeezus’ ilifanikiwa zaidi na kumuingizia kipato kikubwa na kumsaidia kuongeza pato la mwaka kwa asilimia 50.

Angalia orodha kamili:
  1. Dr Dre- $ 620 Million
  2. Jay Z- $60 Million (tie)
  3. Diddy- 60 Million (tie)
  4. Drake – 33 Million
  5. Macklemore & Ryan Lewis 32 Million
  6. Kanye West- 30Million
  7. Birdman – 24Million
  8. Lil Wayne- 23Million
  9. Pharell William -22Million
  10. Eminem- 18Million
  11. Nicki Minaj- 14Million
  12. Wiz Khalifa- 13Million (tie)
  13. Pitbull- 13Million (tie)
  14. Snoop Dogg- 10Million
  15. Kendrick Lamar- 9Million
  16. Luda Cris – 8Million (tie)
  17. Tech N9ne- 8Million (tie)
  18. Swizz Beatz -8Million (tie)
  19. 50 Cent- 8Million (tie)
  20. Rick Ross- 7Million (tie)
  21. J. Cole –7Million (tie)
  22. DJ Khaled- 7Million (tie)
  23. Lil Jon- 7Million (tie)
  24. Mac Miller -7Million
 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Ronaldo Bado Kidume La Liga, Apiga Nne Mguuni Mwake

Ronaldo Bado Kidume La Liga, Apiga Nne Mguuni MwakeMshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro ameendeleza ushajuaa wa kuisaidia klabu ya Real Madrid kupata ushindi katika mchezo wa pili mfululizo wa ligi ya nchini Hispania msimu huu.

Ronaldo alidhihirisha ushujaa wake wakati wa mchezo wa ligi hiyo uliochezwa Estadio Stantiago Burnabeu usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Elche.
Katika mchezo huo mshambuliaji huyo ambaye anashikilia tuzo ya uchezaji bora wa dunia alifanikiwa kufunga mabao manne pekee yake huku bao moja ambalo lilihitimisha ushindi wa mabao matano likifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Wales Gareth Bale.

Hata hivyo Edu Albacar aliiongoza Elche, kupata bao la mapema katika dakika ya 15 kwa njia ya mkwaju wa penati, lakini pamoja na juhudi hizo bado mambo yaliwageukia na kujikuta wakibanjuliwa kwa kipigo cha aibu.
Mchezo mwingine wa ligi ya nchini Hispania uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo ulishuhudia Deportivo de La Coruña wakiendeleza uteja katika ligi hiyo kwa kufungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Celta de Vigo.
Hii leo ligi ya nchini Hispania inaendelea tena kwa michezo kadhaa kuchezwa ambapo;
Almería v Atl Madrid
Eibar v Villarreal
Rayo Vallecano v Ath Bilbao
Granada CF v Levante
Málaga v Barcelona
Sevilla v Real Sociedad

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Rooney Aonyesha Ushupavu Na Kurejesha Salamu Kwa Maadui Wa Man Utd

Rooney Aonyesha Ushupavu Na Kurejesha Salamu Kwa Maadui Wa Man UtdNahodha na mshambuliaji wa klabu Man Utd, Wayne Mark Rooney ameonyesha kuwa na matarajio ya kufanya vizuri msimu huu licha ya kukabiliwa na mwenendo mbovu wa kuanza ligi kuu ya soka nchini
Uingereza chini ya meneja kutoka nchini Uholanzi Louis van Gaal.
Rooney, ametoa msisitizo huo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo ameandika ana mtazamo tofauti na jinsi ambavyo watu wanavyo wachukulia Man Utd, kutokana na matokeo mabaya ya mwishoni mwa juma lililopita baada ya kufungwa na klabu ya Leicester City mabao 5-3.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ameongeza kuwa kila anapowangalia wachezaji waliopo kwenye chumba cha kubadilishia nguo, anaona vipaji  ambavyo vikichanganywa na umakini wa meneja wao hana shaka kwamba klabu hiyo itapata mafanikio.
Man Utd, imekuwa haifanyi vizuri tangu mwanzoni mwa msimu huu na mpaka sasa imeshapoteza michezo miwili, kutoka sare mara mbili na kushinda mmoja.

Video Mpya: Wiz Kid- In My Bed

Video Mpya: Wiz Kid- In My Bed Video Mpya: Wiz Kid- In My Bed Wizkid ameachia video mpya ya wimbo wake ‘In My Bed’ wenye shots matata akiwa na mrembo anamshawishi apumzishe mwili wake kwenye kitanda chake. Angalia hapa:

Video: Marekani yatoa video inayoonesha mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS nchini Syria

Video: Marekani yatoa video inayoonesha mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS nchini Syria  Video: Marekani yatoa video inayoonesha mashambulizi ya anga dhidi ya ISIS nchini Syria Marekani na washirika wake wamelenga kushambulia na kutokomeza kundi hilo linalotekeleza mauaji na Makao Makuu ya Ulinzi, Pentagon Marekani imetoa kipande cha video inayoonesha jinsi walivyotekeleza na kufanikisha mashambulizi ya kwanza nchini Syria dhidi ya kundi linalojiita Islamic State Of Syria and Iraq (ISIS). September 23 jeshi la Marekani lilitekeleza mashambulizi ya anga katika makao makuu ya kundi hilo Ar Raqqah, Syria. kuwachinja raia wa Marekani na Uingereza huku wakionesha katika vipande vya video.

SWANSEA YAIFUMUA EVERTON 3-0 KOMBE LA LIGI

Mholanzi Marvin Emnes akipongezwa na Jonjo Shelvey baada ya kuifungia Swansea bao la tatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Everton katika Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup jana usiku. Mabao mengine ya swansea yalifungwa na Nathan Dyer na Gylfi Sigurdsson.

Who's Bad: Ali Kiba anapendwa zaidi Uingereza kuliko Diamond?


Mabishano ya mashabiki kuhusu ni nani mkali kati ya Diamond na Ali Kiba ulionekana kufifia kwa muda kidogo kwenye media lakini ukweli ni kwamba pressure iliyoko mitaani kiuhalisia kwa wasanii hawa inafanya mada hiyo kutoepukika kirahisi.
Mtandao wa Bongo5 umeibua gumzo jingine baada ya kufanya mahojiano na promota wa muziki na filamu anaefanya kazi zake nchini Uingereza, Hadija Seif, maarufu kama Dida Fashion na alisema nchini humo Ali Kiba anapendwa zaidi ya Diamond.
Sio sasa hivi tu, tangu zamani to be honest kwa UK Alikiba yupo juu zaidi.  Sijui kwanini lakini kwa watu wenyewe ukisema labda kati ya Ali kiba na Diamond hapo nani aletwe, honestly watu wa UK yaani Ali kiba sijui aliwafanya nini lakini Alikiba UK is the best.” Alisema promota huyo.
Hata hivyo, ripoti hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti mashabiki wa muziki.
Mtu mmoja anaetumia jina la Blacksailors Jangombwe kwenye Facebook, yeye ni mtanzania anaeishi Uingereza ambaye alitofautiana na ripoti ya Dida.
Hiki ndicho alichoandika:
 “Please Dida Please!!. If you can't afford to hire someone, doesn't mean he's not popular then the one you just mention. kuwa mkweli uliweza kumleta diamond UK before but now you can't,because he's very expensive. Sasa unaposema UK wanampenda fulani then fulani kwaushahidi upi??. have u done a survey If YES when and which county in UK. Watu wamejaa kwenye holli waiting up to 5:00 am. Unafikiri angekua huyo unaemtaja wewe, Nani UK ungemueka asubiri mpaka saa 11 alfajiri Common Dida. Msema ukweli ni mpenzi wa mungu. Better to try another way to promote DIDA ENT. Northampton peoples know better than thaaaaaaat!!!!. Common sister you know we always love you and support you,don't do that, TheTruth is matter.”

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

CAF yaipiga JS Kabylie marufuku



Klabu ya Algeria JS Kabylie imepigwa marufuku kushiriki mashindano yeyote kwa miaka miwili.
Shirikisho la soka la barani Afrika CAF limefikia kauli hiyo baada ya kuuawa kwa mshambulizi wa Cameroon Albert Ebosse uwanjani mwezi uliopita.
Ebosse alikufa baada ya kupurwa na jiwe baada ya mechi ya ligi kuu ya Algeria.
Marufuku hiyo inatarajiwa kuathiri pakubwa Kabylie ambayo ilikuwa imefuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita.
Ebosse alikufa baada ya kugongwa na jiwe kichwani baada ya mechi ya ligi
Caf vilevile imeratibua kuanzisha tuzo kwa heshima yake Ebosse.
Klabu hiyo tayari imepigwa marufuku ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu wote wa 2014-2015 .
Aidha mashabiki wake hawawezi kushuhudia mechi yake yeyote nyumbani wala ugenini.
 

USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Abu Qatada hana hatia ya ugaidi

Mahakama nchini Jordan haijampata na hatia ya tuhuma za kigaidi Mhubiri wa kiisilamu anayesemekana kuhubiri itikadi kali Abu Qatada.
Jopo la majaji wa kiraia waliokuwa katika mahakama hiyo, hawakumpata na hatia yoyote bwana Qatada kutokana na madai kuwa alihusika na njama iliyotibuliwa ya kushambulia sherehe za mwishoni mwa mwaka 2000.
Uamuzi huo umetolewa baada ya Abu Qatada kutopatikana na hatia mwezi Juni katika kosa lengine la kupanga njama ya mashambulizi mwaka 1998 nchini Jordan.
Abu Qatada alitimuliwa kutoka Uingereza mwezi Julai mwaka 2013 kwa madai ya kueneza itikadi kali.

Jeshi labadili kauli kuhusu wanafunzi

Jeshi la Nigeria limekanusha taarifa ya awali kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule waliotekwa nyara kutoka Chibok na wapiganaji wa Boko Haram, wameachiliwa.
Msemaji wa jeshi nchini Nigeria, Meja Generali Chris Olukolade, ameambia BBC kuwa wanawahifadhi wasichana kadhaa lakini akakana kuwa wasichana hao ni baadhi ya wale waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram kutoka Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na Boko Haram kutoka shule ya mabweni Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno.
Utekaji nyara huo ulisababisha ghadhabu kote nchini Nigeria na duniani kote kiasi cha kusababisha kampeini ya kutaka kuokolewa kwa wasichana hao kwenye mitandao ya kijamii.
Maandamano yenye kauli mbiu, (#BringBackOurGirls) yaliandaliwa kutoa wito kwa watawala kuongeza juhudi za kuwanusuru wasichana hao,
Muda mfupi baada ya kuwateka nyara,Boko Haram, ilitoa kanda ya video wakisema kuwa wasichana hao wataachiliwa tu ikiwa serikali itakubali kuwaachilia wapiganaji wa kundi hilo ambao wanazuiliwa.
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ripoti ambazo hazijathibitishwa zikisema kuwa serikali ya Nigeria imekuwa ikifanya mazungumzo na Boko Haram, kubadilishana wasichana hao na wapiganaji wao wanaozuiliwa.
Tangu kutolew kwa amri ya kutotoka nje nyakati za jioni, katika eneo la Kaskazini Mashariki kwa lengo la kutatiza harakati za Boko Haram, kundi hilo limekuwa likiendeleza mashambulizi.
Wanawake wengi na watoto, wakiwemo wasichana wamekuwa wakitekwa nyara.
Awali, Generali Olukolade aliambia BBC kuwa shughuli inaendelea ya kuwaokoa wasichana hao na kwamba baadhi ya wasichana haio wako salama katika kambi za jeshi.
Hata hivyo msemaji huyo baadaye alisema kuwa jeshi linajaribu kuwatambua wasichana hao ambao wako chini ya ulinzi wa jeshi lakini hawakurejea kutoka Chibok.

Balozi wa zamani Vatican matatani

Vatican imempa kifungo cha nyumbani aliyekuwa balozi wake katika jamuhuri ya Dominica Jozef Wesolowski.
Inaarifiwa hatua hiyo imechukuliwa dhidi ya balozi huyo wa zamani kwa kosa la kuwadhalilisha watoto kijinsia.
Kasisi huyo wa zamani aliondolewa wadhifa wake mwezi Juni baada ya jopo la viongozi wa kanisa kumpata na hatia ya kuwalawiti watoto wavulana wakati akifanya kazi katika Jamuhuri ya Dominica.
Kesi yake itasikilizwa na mahakama ya uhalifu ya Vatican. Itakuwa kesi ya kwanza kumhusisha afisa wa ngazi ya juu kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Wesolowski, ambaye asili yake ni kutoka Poland, alihudumu kama balozi wa Papa katika jamuhuri hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Msemaji wa Vatican, alisema kuwa kukamatwa kwa askofu huyo ni mapenzi ya papa kwamba kesi kama hiyo inayozua hisia isikilizwe kwa haraka bila kuchelewa.
Papa Francis ameahidi kufanya msako dhidi ya makasisi na wafanyakazi wa Vatican, ambao huwadhulumu watoto wadogo akifananisha vitendo vyao kama vya kishetani.
Mwaka jana aliweka sheria kali dhidi ya watuhumiwa wa udhalilishaji wa watoto katika Vatican.
Msemaji wa Vatican, alisema kuwa uamuzi wa kumpa kifungo cha nyumbani askofu huyo, badala ya kumzuilia katika kituo cha polisi, ulifikiwa kutokana na afya yake.
Kesi ya Wesolowski inatarajiwa kusikilizwa baadaye mwaka huu.

Tuesday, September 23, 2014

Obama aapa kuangamiza Islamic State

Rais wa Marekani Barack Obama amesema Marekani itashambulia kundi linalojiitaa Islamic state kote nchini Syria na Iraq ili kuwanyima kabisa makao ya kujificha .
Bw Obama amesema kushiriki kwa mataifa kadhaa ya kiarabu katika mapambano hayo kunaonyesha wazi hivyo si vita vya Marekani pekee bali wao ni sehemu ya muungano wa mataifa yanayopigana na kundi hilo liitwalo pia ISIL.
Pia amekiri kuwa mashambulio hayo yamelenga pia wale aliowataja kuwa wanamgambo sugu wa al Qaeda wa kundi liitwalo Khorasan ambao anasema wanalenga kuishambulia Marekani.
Nazo taarifa za jeshi la Marekani zasema malengo ya mashambulio yaliyofanywa yametimia.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa wakifanya mauaji na utekaji nyara 
Wanamgambo kadhaa wa IS wameripotiwa kuuliwa japo vifo vya raia pia vimeripotiwa.
Mapema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Alexander Lukashevichy amesema mashambulio yoyote dhidi ya ISIL ni sharti yazingatie sheria za kimataifa.
Kadhalika Obama, amesema kuwa kuhusika kwa nchi za kiarabu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria ni dalili toshja kuwa vita hivi sio vya Marekani pekee.
Obama amesema ataendelea kukusanya jeshi la kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Saudi Arabia, Milki za kiarabu,Jordan na Bahrain zote zilituma ndege za kijeshiu katika opereshei hiyo.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

AUDIO: Sikiliza sauti ya T.I akithibitisha kutua Dar kwenye makamuzi ya Serengeti Fiesta 2014

Maswali mengi tuliyokuwa tukijiuliza juu ya msanii gani wa kimataifa atakae dondoka Dar kwa ajili ya finali za tamasha la Fiesta leo hii yamepata majibu. Akitangazwa kupitia kipindi cha XXL akiwepo Fetty na B12, watangazaji hao walihesabu mpaka kuanzia 10 mpaka 0 ilimradi tu kuwapa kiraruraru wasikilizaji wao na mwisho wa siku wakamtangaza msanii wa kimataifa T.I kutoka Marekani kuwa ndie atakaefanya makamuzi ndani ya Serengeti Fiesta 2014, itakayofanyika tarehe 18 October 2014 kwenye viwanja vya Leaders Club...msikilize hapa chini akithibitisha uwepo wake


USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Polisi mkoani Kigoma wakamata kazi feki za wasanii, laptop na vidhibiti vinginevyo

Hivi karibuni polisi mkoani Kigoma chini ya RPC Frasser Kashai wamefanya kitendo cha kishujaa baada ya wiki hii kutonywa na raia wema kuwa kuna watu wanarudufisha kazi za wasanii. Baada ya habari hizi kuwafikia. polisi wakavamia eneo la tukio na kukuta vidhibiti kibao, zikiwemo CD zaidi ya 200, Laptop 4 na Desktop kama 5 na tayari mchakato wa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao umekamilika kinachofata ni sheria kuchukua mkondo wake Akiongea leo hii RPC Frasser hiki ndicho alichokisema "ee ni kweli nilikamata hizo kazi zilizodurufiwa za wasanii, ni taarifa tu ambazo tunazipata katika shughuli zetu za udhibiti wa makota, vija tukawatuma wakaenda kukamata na tukawafikisha mahakamani, kulikuwa na CD zaidi ya 200, laptop kama 4 na desktop kama tano hivi na vitu vitu kama hivyo navikumbuka kichwani kiasu tu , sina muda mrefu hapa ila hivyo vitu vinakamatwa mara kwa mara inaonyesha bado wananchi hawajazoea hili, sehemu mbali mbali nilikopita mwamko bado lakini huwa tunakamata, polisi huwa tunakama"

MWALIMU AKUTWA AMEFUNGWA MINYORORO KANISANI


Ndugu wa mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35) ambaye ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo kwa miezi nane mfululizo. GPL(P.T)

Mwalimu Galus Focus Nguruwe akiwa amefungwa mnyororo
Kwa mujibu wa dada wa Galus, Piencia Focus, ndugu yao huyo alichukuliwa na mke wa mtoto wa dada yao waliyemtaja kwa jina la Doreen kutoka Songea mkoani Ruvuma Januari, mwaka huu bila kuwataarifu ndugu, jambo lililowafanya wamfuatilie na kugundua alipelekwa kwenye kanisa hilo kwa madai ya kufanyiwa maombi.

Dada wa Galus, Piencia Focus akiwa kanisani hapo
Dada huyo alisema kuwa aliamua kumtafuta ndugu yake hasa baada ya kupata taarifa kuwa aliko amekuwa akishinda  huku amefungwa mnyororo mguuni,  hali inayomfanya ajisaidie na kula papohapo.
“Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa  akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro,” alisema Piencia Focus.

Kaka wa Galus,Peter Focus akizungumza na waandishi wa habari.
Naye kaka wa Galus, aliyejitambulisha kwa jina la Peter alisema baada ya kupata taarifa kwamba mdogo wake yupo kwenye kanisa hilo aliamua kufika kwa ajili ya kumchukuwa kistaarabu lakini cha kushangaza alijikuta akiangukia kwenye mikono ya waumini hao wakidai yeye ni gaidi na wakamkwapulia fedha zake.
Peter alisema alipoachiwa alikimbilia Kituo cha Polisi Wazo Hill ambapo alifungua jalada lenye Namba za Kumbukumbu WH/RB/6364/14 WIZI TOKA MAUNGONI.

Waumini wa kanisa hilo wakijibizana na ndugu wa Galus kanisani hapo.
Peter alisema alilazimika kuungana na dada yake kwa kushirikisha na vyombo vya usalama ambapo walifika kanisani hapo kwa mara nyingine ili kumkomboa ndugu yao na kuwatia mikononi waumini waliomwibia fedha zake.
Waandishi wetu waliokuwa karibu na eneo hilo walizinyaka taarifa hizo na kufika kanisani hapo ambapo waliwashuhudia ndugu hao wakiwa na polisi wakimchukuwa mmoja wa watuhumiwa waliodaiwa kumshambulia Peter na kuondoka naye.

Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship kwa muonekano wa mbele.
Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kitendo cha polisi hao kumwacha Galus akiwa bado amefungwa kwenye nguzo na mnyororo kanisani hapo wakidai watamfuata baada ya kumpeleka mtuhumiwa wa unyang’anyi kituoni, jambo ambalo halikuwa la kweli kwani hawakufika kwa siku hiyo.
Waandishi wetu walishuhudia timbwili la aina yake kanisani hapo kati ya waumini wa kanisa hilo na ndugu wa Galus waliorejea kwa lengo la kumchukuwa ndugu yao baada ya awali kumpeleka kituoni mtuhumiwa wa kumshambulia Peter.
Waandishi wetu walipoomba kuzungumza na uongozi wa kanisa hilo ilishindikana na kujikuta wakishambuliwa kwa maneno huku wakitakiwa kuondoka mara moja katika eneo la kanisa hilo.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Video: Hatimae Beyonce aonyesha picha yake akiwa na mimba ya Blue Ivy amepozi mtupu na Jay z, Video ya harusi yao ambayo haikuwahi kuonekana popote...

Baada ya tetesi kibao kusambaa juu ya ndoa yao wengi wakidai kuwa ipo mashakani na hata kusemekana kuwa si kweli kuwa Beyonce ndie aliemzaa Blue Ivy, Beyonce na Jay Z wamejaribu kuzizima tetesi hizo baada ya kujumusiha video zao binafsi (home videos) wakati wa usiku wa mwisho wa tua yao pamoja "On The Run Tour"
Kipande hicho cha video chenye dakika 6 kilionekana kwenye background wakati wawili hao wakiimba hit song zao "Young Forever" na "Halo" wakionekana katika sehemu mbali mbali waki-enjoy wakati wa mapunziko, wakiwa kwenye boat na ku -share champagne.
Video ya siku ya harusi yao(2008) ambayo haijawahi kuonekana imechanganywa katika mix ya video hizo pia video ya wawili hao wakichora tattoo zinanofanana kwenye vidole vyao


 Video hiyo iliendelea kuonyesha video ya karibu ya ujauzito wa Beyonce akiwa mtupu mbele ya Jay Z huku Jay akiwa amekunja mikono yake mbele ya tumbo la Bey.hata kuna vipande vya hospitali vinavyomuonyesha Bey akiwa amempakata mtoto wake dakika kadhaa baada ya kujifungua.
Akiongezea juu ya tetesi zinazoendelea, Jay alibadilisha mashairi ya wimbo wake Beach Is Better, kutoka "I replace it with another one" na kuwa "Cause she is pregnant with another one" wakati huo huo sio Bey wala Jay wamethibitisha kuwepo kwa ujauzito wa mtoto wa pili.
Wawili hao walimaliza tour yao na show mbili za Paris zilizokuwa sold out.
 
 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Nu Joint: Bibo feat Madee - Wanaona Gere

MBUNGE KESSY ASIPIGWE, AJIBIWE HOJA ZAKE



Mbunge wa Nkasi (CCM),  Ally Kessy akisisitiza jambo.
Mbunge wa Nkasi (CCM),  Ally Kessy wiki iliyopita  alilazimika kusindikizwa na askari wa Bunge la Jamhuri kuondoka katika viwanja vya eneo hilo kumnusuru na hasira za wajumbe kutoka Zanzibar waliokerwa na mchango wake kuhusu masuala ya Muungano.
Kessy alisimama bungeni hapo kutoa mchango wake kuhusu Katiba ya Jamhuri akijikita zaidi katika suala la muundo wa Muungano na kusema kwamba Zanzibar inabebwa na Tanganyika.
Nimnukuu, alisema: “Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanganyika inabeba mzigo mkubwa ambao haubebeki, hapa tunahudumia wabunge 83 kutoka Zanzibar ambao wanatibiwa wao na wake zao na watoto kwa gharama za Tanganyika wakati hawachangii.”
Aliongeza kuwa haiwezekani kwa Tanganyika kubeba mzigo mkubwa kama huo wakati katika Jimbo lake la Nkasi wananchi wanalia na shida ya maji.Alisema katika kamati yao Namba Moja, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu alitoa semina iliyoonyesha kuwa Zanzibar haichangii chochote kwenye Serikali ya Muungano na kuwa hata mishahara wakati mwingine wanategemea Tanganyika.
Kessy alisema wananchi wakilijua jambo hilo, wataikataa katiba inayopendekezwa na kuitupilia mbali kwa kuwa inatoa upendeleo kwa Wazanzibari na kuikandamiza Tanganyika.GPL (P.T)
“Mimi naweza kuwa na wanawake sita, nikazaa nao lakini kila mtoto anaendelea kutunzwa na baba yangu, jambo kama hili halivumiliki hata kidogo japo najua kuwa ukweli unawauma,” alisema huku baadhi ya wajumbe wakipaza sauti wengine kumpinga na wengine kuomba mwongozo wa mwenyekiti.
Lakini ninachotaka kusema hapa ni kwamba wananchi wengi wa Tanganyika niliozungumza nao katika utafiti wangu usio rasmi wanaungana na mbunge huyo.
Hapa Dar es Salaam baadhi ya wakazi wanasema iweje Zanzibar yenye watu milioni moja na ushee wawe na wabunge 83 wakati jiji lao lina wakazi zaidi ya milioni nne na lina wabunge wasiozidi kumi?
Alipinga suala la Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa Muungano kwa maelezo kuwa katika mfumo wa vyama vingi jambo kama hilo haliwezekani na kuhoji itakuwaje awe makamu wa kwanza wa rais wakati hajachaguliwa na wananchi wa Tanzania Bara?
Baada ya kauli hiyo, kelele za wajumbe kutoka Zanzibar ziliongezeka baadhi wakisimama na kuwasha vipaza sauti kumshambulia Kessy hivi: “Chizi huyo, chizi huyo, hafai kwanza ni Mwarabu,” zilisikika sauti huku nyingine zikimtaka aombe radhi.
Ukweli ni kwamba alichokizungumza Kessy ndizo kero za muungano kwa upande wa Tanganyika. Kati ya watu 50  niliowauliza jijini Dar kuhusiana na kauli hizo, ni wawili tu waliopingana naye, hivyo ni dhahiri kwamba kauli yake inapaswa kutazamwa.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kwamba wachache wakitokea na kutoa wazo ambalo baadaye linaweza kuleta vurugu, ni bora likakubaliwa kama halina madhara. Hivyo hayo ya Kessy yatazamwe na yasipelekwe kisiasa.
Sikuona sababu za wajumbe kutoka Zanzibar kumshambulia Kessy wakati aliyesema hayo ni Gavana wa Benki Kuu, Bwana Ndulu yeye alikuwa akirudia na ndiyo maana akasema hayupo tayari kuomba radhi.
Alidai Ndulu alikuja katika kamati na akasema kwamba tangu kifo cha Abeid Karume (rais wa kwanza wa Zanzibar), Zanzibar hawajawahi kuchangia muungano, hili lilikuwa ndilo la msingi la kulijadili kama ni kweli au ni uzushi na siyo kuzomea na kutaka kumpiga mtoa hoja.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

Tahadhari kwa wanaotumia Sukari nyingi

Wataalamu wa afya wanatahadharisha kuwa juhudi zaidi zinahitajika kupunguza kiwango cha Sukari kinachotumiwa na watu.
Shirika la afya duniani kwa ushirikiano na washauri wa maswala ya afya nchini Uingereza, wamependekeza kupunguza viwango vinavyopendekezwa vya kutumia sukari mwilini.
Ushauri mpya unasema kuwa kiwango kinachostahili cha Sukari mwilini ni asilimia 5 kutoka asilimia 10.
Lakini utafiti mbadala unasema kwamba kiwango kinachofaa hakipaswi kuwa zaidi ya asilimia 3.
Watafiti wanasema kuwa ushauri huu mpya unahitajika ikizingatiwa gharama ya matibabu kwa sekta ya afya hasa matibabu ya magonjwa ya Meno.Chanzo: BBC
Wanasema kuwa Sukari ni kiungo muhimu zaidi katika kuchochea magonjwa ya Meno kwa sababu ya hilo, ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika.
Utafiti unaonyesha kuwa kutumia kiwango kikubwa cha Sukari mwilini kunaongeza uwezekano wa meno kuoza na kuharibika hususan kwa watoto.
Matibabu ya magonjwa ya Meno hugharibu nchi zilizostawi kati ya asilimia 5 na kumi ya matumizi ya pesa za matibabu.
Wataalamu wanasema kuwa hatua zinapaswa kuchukuliwa kwa haraka.
'Kodi kwa Sukari'
Wataalamu wanataka serikali kudhibiti upatikanaji wa mashine za kuuza soda na vinywaji vingine vyenye sukari na hata kuyaondoa katika maeneo ya shule na hospitali.
Pia wanasema kuwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukari vinapaswa kuwekwa vibandiko na serikali kuvitoza ushuru mkubwa.
Wanasema kuwa swala la watu kutumia sana Sukari ni tatizo kubwa kwa umma.
Licha ya hatua kuchukuliwa kupunguza matumizi ya Sukari, takwimu zinaonyesha kuwa watu wengi bado wanatumia kiwango kikubwa cha Sukari.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

WASANII WASISITIZWA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII


Mdau wa Sanaa Henry Mdimu (Kulia) akisisitiza umuhimu wa kuwa na mitandao ya kijamii kwa wasanii (hawapo pichani) katika Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Kushoto ni Afisa Sanaa wa BASATA, Augustino Makame.

Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kulia) akisisitiza jambo kwa Wasanii (Hawako pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau wa Sanaa Henry Mdimu na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.(P.T)

Wadau wa Sanaa pamoja na Wasanii wakipata elimu kuhusu Nafasi ya Mitandao ya Kijamii katika Kukuza Sekta ya Sanaa kwenye mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.
Na Mwandishi Maalum
Wasanii wamesisitizwa juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani waandaaji wa matamasha na matukio mbalimbali ya kisanaa sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiitumia katika kuwapa kazi.
Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam, mdau wa Sanaa Henry Mdimu alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona wasanii wakitumia kurasa zao kuonesha mambo binafsi kama ya mapenzi na matusi wakati zinapaswa kutumika kwa ajili ya kazi zao za Sanaa na kuwasiliana na mashabiki wao.
Alisisitiza kwamba si kila kitu kinapaswa kuwekwa kwenye kurasa za kijamii za wasanii na kwamba lazima wasanii wajifunze kutenganisha maslahi au masuala yao binafsi dhidi ya yale ya wapenzi wao na kwamba Sanaa iko kwa ajili ya walaji na si wasanii pekee.
“Wasanii hawana budi kuelewa kuwa hawatengenezi sanaa au kurasa za mitandao ya kijamii kwa ajili yao. Wanaitengeneza ili kuwasiliana na mashabiki wao kuhusu kazi wazifanyazo na kutafuta fursa za masoko na kazi nje. Lazima waelewe mapromota wa kimataifa hutumia sana kurasa hizi katika kutoa fursa” alisisitiza Mdimu.
Aliongeza kwamba, msanii yeyote anayefanya kazi ya Sanaa kama kazi yake lazima afikirie kutumia mitandao hii ya kijamii kiweledi katika kujitangaza kwani kutokufanya hivyo ni bora kufanya kazi nyingine maana hiyo ndiyo njia kuu kwa sasa ya kujitangaza na kupata fursa za maonesho mbalimbali ya kimataifa kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame alisema kwamba Baraza limekuwa mstari wa mbele kusisitiza matumizi sahihi ya teknolojia za kupashana habari muiongoni mwa wasanii na kwamba sasa ni muda wa wasanii kuona umuhimu wa mitandao hii ya kijamii na kuitumia ipasavyo katika kukuza Sanaa zao.

 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA 

TANZANIA YASISITIZA VIPAUMBELE VYA KITAIFA VIPEWE UMUHUMU


Mhe. Waziri Fatma Fereji akiwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati wa ufunguzi wa Kikao Maalum wa ICPD ambapo Waziri Fereji aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo.

Kutoka kushoto ni Balozi Ramadhan Mwinyi, Waziri Fatma Fereji wakiwa na Mwakilishi kutoka Ofisi za UNFPA ambaye aliwahi pia kufanya kazi nchini Tanzania akimpongeza Waziri baada ya kutoa mchango wa Tanzania na kulia kabisa ni Dkt. Joyceline Kaganda.GPL(P.T)

Mhe. Waziri Fatma Fereji kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akizungumza kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kikao Maalum cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Jumatatu ambapo wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali kutoka nchi 193 walikutana kutathimini Mpango wa Utekelezaji walioupitisha miaka 20 iliyopita huko Cairo, Misri kuhusu uboreshaji wa maisha ya watu na masuala yahusuyo Idadi ya Watu. Mhe. Fereji ni sehemu ya Ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


 USIPITWE NA HABARI MBALIMBALI ZIKIWEMO ZA SIASA NA NYINGINE NYINGI NI HAPAHAPA WWW.MAXWELLPAIN.BLOGSPOT.COM ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG PENDWA