Mshambuliaji
wa zamani wa klabu ya FC Barcelona na Chelsea Samuel Eto’o amekamilisha
usajili wa kujiunga na Klabu ya Everton pamoja na kwamba alikuwa
akikaribia kujiunga na Liverpool.
Everton amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo nahodha huyu wa timu
ya taifa ya Cameroon ameripotiwa kusononeshwa na uhamisho wake kwenda
Liverpool kufeli wakati akiwa tayari alishafanya mpaka vipimo vya afya.
kwenye sentensi nyingini ni kwamba Eto’o anatarajiwa kuanza kuichezea
Everton weekend hii kwa mechi dhidi ya Chelsea ambayo aliitumikia msimu
uliopita.
0 comments:
Post a Comment