Taarifa
zilizotoka saa kadhaa zilizopita zilionyesha kwamba kati ya Wagonjwa
nane waliokutwa na Ebola huko Congo DRC, wawili kati yao wamefariki
dunia.
Taarifa hizi zimeendelea kuwashtua na kuwafanya majirani kuzingatia
tahadhari ambapo mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya amesema ‘pamoja na
tishio la ugonjwa huu kwamba uko DRC Congo lakini DRC ya mbali sana
kule kaskazini wanakopakana na Afrika ya kati na Sudan, tumeanza
kuchukua tahadhari kwenye mipaka yetu manake binadamu wanatembea na
maingiliano ni makubwa’
‘Kuanzia leo nimemuagiza katibu tawala wa mkoa magari yote yenye
uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu wamesharudi nyumbani
yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo licha ya
kuweka vipeperushi’ – Machibya.
John Ndunguru ambae ni katibu tawala wa mkoa amesema ‘Kwenye
hospitali zetu wameshatenga chumba maalum kama atatokea mgonjwa yeyote
manake inabidi Wagonjwa hawa wawekewe kinga au wigo kwa siku 48,
vilevile wizara ya Afya imeahidi kutuletea vifaa vya kutosha hasa vya
kinga na dawa mbalimbali, tayari maafisa Afya wako hata uwanja wa ndege
kukagua kila anaeingia’
Wednesday, August 27, 2014
Home »
» Baada ya wawili kufa kwa Ebola Congo DRC, Mkuu wa mkoa Kigoma ametoa hii
0 comments:
Post a Comment