Sio
kitu kigeni kuona watu wenye umri zaidi ya miaka 18 wanakunywa Pombe
wanalewa na hata pombe hiyo kugharimu maisha yao ila sio kawaida
kukutana ama kuona mtoto wa miaka kati ya 14-17 ni mlevi wa kupindukia
na mtumiaji pia wa dawa za kulevya.
Ripoti
mpya iliyotolewa na Mamlaka ya kudhibiti vileo nchini Kenya (NACADA)
inaonyesha kwamba ni watoto zaidi ya MILIONI MOJA nchini humo wenye umri
kati ya miaka 14-17 ambao ni watumiaji wakubwa wa pombe na dawa za
kulevya.
Kenya Julius Kepkoech amesema mwenyekiti wa NACADA John Mututho
ameisema hii wakati alipowatembelea Wanafunzi 16 waliokamatwa wakiwa
wamelewa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo sasa wamefikishwa kwenye
Mahakama ya Baricho.
Hakimu
mkuu wa Baricho Hezekiah Keago ameamuru Wanafunzi hao baadhi kurudishwa
mikononi mwa wazazi ili kufanyiwa ushauri nasaha lakini pia vilevile
Wanafunzi wengine waliobakia kati ya hao wamehukumiwa kwenda jela ya
Watoto Muranga.
Ushahidi
uliotolewa Mahakamani umeonyesha kwamba hawa Wanafunzi ambao
wamekamatwa kwa ishu ya pombe, walihusika kuinywa pia pombe iliyopigwa
marufuku nchini Kenya ambayo ina kemikali hatari kwa afya na iliua zaidi
ya watu mia moja.
Saturday, August 30, 2014
Home »
» Home » stori kubwa » Uliipata hii ya Wanafunzi Kenya kupelekwa Mahakamani baada ya kukutwa wamelewa? Uliipata hii ya Wanafunzi Kenya kupelekwa Mahakamani baada ya kukutwa wamelewa?
0 comments:
Post a Comment