Search This Blog

Sunday, August 31, 2014

Huyu ndio mshindi wa Super Nyota Diva kutoka Moshi

Ule mchakato wa kutafuta wasanii wa kike wenye uwezo na kipaji cha kuimba au kuchana, Super Nyota Diva, umefanyika mkoani Moshi na mshindi amepatikana 
Super Nyota Diva imefanyika katika ukumbi wa Club Aventure ambapo licha ya kuwa na washiriki wachache waliojitokeza, vipaji vyao ni vikubwa sana. 
Kama ambavyo nilitegemea, kulikuwa na wale ambao wanafanya hiphop na kuimba pia, naushindani ulikuwa ni mkubwa pamoja na kuwa ni wachache.

Siamerry ndio Super Diva anaewakilisha Moshi, anafanya hiphop na ndio iliyompelekea kushinda kwake, ana uandishi mzuri wa mistari na flow iliyoshiba. Siamerry ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa pili (UDOM)

Majaji ni Kenoo ambae ni producer kutoka Black Market Music Production na Fetty 


0 comments:

Post a Comment